Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga akipokea Tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Kamishna wa Jeshi hilo anayehusika na Rasilimali Watu, DCF Athuman Nassa (Kulia) iliyotoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kushoto ni Kamishna wa Utawala na Fedha Mbaraka Semwanza, ndc na Kamishna wa Usalama kwa Umma Jesuald Ikonko aliyesimama upande wa kushoto kwa Kamishna Jenerali.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetunukiwa tuzo ya Utendaji Bora katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Tuzo hiyo ya Nafasi ya 3 imetolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: