Kaimu Mkuregenzi Idara ya Miundombinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Ntonda Kimasa mwenye kofia nyeupe, akitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi wa ukarabati wa skimu ya Idudumo Mhandisi Jumbe Tibori mwenye kofia  nyekundu kushoto, wakati wa ukaguzi wa kazi inayoendelea katika skimu hiyo.

Picha ikionesha sehemu ya mfereji mkuu wenye urefu wa kilomita mbili utakaopeleka maji mashambani ukiwa katika atua ya ujenzi.

(Habari na Picha na Kitengo cha Habari na Mawasilino.)

NZEGA - TABORA

 

Wahandisi wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini wametakiw a kusimamia kazi za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya miradi kwa umakini na ueledi mkubwa kwani,kazi hizo zinatakiwa kufanyika kwa wakati kulingana na mkataba kwa wakandarasi na hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa mkandarasi ambaye atafanya kazi kwa kuchelewa na chini ya kiwango.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki, na Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Miundombinu kutoka  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Ntonda Kimasa, alipokuwa katika skimuyaKilimo cha Umwagiliaji Idudumo wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Mhandisi Kimasa alisema, Serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 700 fedha za ndani,kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao una bwawa na utahusisha kuboresha mfereji mkubwa wenye urefu wakilomita mbili pamoja na mifereji mingine mitano ya upili yakupeleka maji mashambani.

BaadayakufanyaukaguziwaujenzinaukarabatikatikaskimuhiyoMhandisiKimasaalisema“Kwa ujumlakaziinaendeleavizurinaninaaminikaziitakamilikanamkandarasiataikabidhikwawakati.” Alisisitiza.

Akiongea kwa niaba ya wakulima wa chama cha umwagiliaji Idudumo, Bwana Stefano Honoli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya ujenzi,amemshukuru Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo,kwa jitihada anazofanya katika kuboresha sekta yakilimo cha umwagiliajinakuiombaserikaliyaawamuyasitakuendeleanaawamunyingineyaukarabatikatikaskimuhiyokwakutoamafunguzaidiyafedha, kwaniskimuhiyoinauwezowakulishamkoamzimawaTabora.

Kazi ya ukarabati wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji Idudumo inayofanywa na mkandarasi mzalendo M/S Explicit Main ConstractorsLtd.inategemewa kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu,na utasaidia wakulima kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji katika kipindi chote cha mwaka.

 


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: