Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI akiwa na timu kutoka DMI tayari Kwa maonyesho ya NACTVET katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama Mjini atembelea banda la DMI.Bi. Winfrida Ngallu, mwanafunzi wa Marine Engineering, mwaka wa tatu akitoa elimu kuhusiana na taaluma ya ubaharia.Capt. Azan Azan kutoka chuo cha DMI akitoa elimu ya kujiokoa wakati wa dharula melini.Umati wa wananchi umefurika katika banda la DMI wakipatiwa elimu ya bahari.Watumishi kutoka chuo cha DMI wakijioanga kutoa huduma Kwa wananchi katika viwanja vya Jamhuri - Dodoma.

Prof. Zacharia Nganilo, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) atembelea banda la DMI.

***************

Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) kimeshiriki maonyesho ya Vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Juu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Maonyesho hayo ya siku Saba yameanza tarehe 07  - 13/06/2022 yamejumuisha Vyuo mbalimbali nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt. Lucas Mwisila ametoa wito kwa umma wa Tanzania kujiunga na Chuo hicho kutokana na fursa zilizopo katika tasnia ya bahari.

Dkt. Mwisila amesema Kwa sasa dirisha la udahili lipo wazi kwa ngazi ya Cheti na Diploma, hivyo anawakaribisha watanzania na wasio watanzania kujiunga na chuo cha bahari Dar es Salaam.

Chuo cha bahari dar es Salaam kinatoa kozi za ubaharia zikiwemo Uendeshaji wa meli (Unahodha), Uhandisi wa meli, Usimamizi wa masuala usafirishaji na lojistiki, Uhandisi wa mafuta na gesi na nyingine nyingi ambazo zinatolewa Kwa ngazi ya Cheti, diploma, digrii na Uzamili.

Aidha chuo kinatoa kozi fupi pamoja na kozi za umahiri kuhusiana na tasnia ya bahari.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kozi zitolewazo na chuo cha DMI unaweza kutembele tovuti ya chuo www.dmi.ac.tz au unaweza kupiga simu 0688 941 921/ 0716 898 037
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: