Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa wakishuka kwenye kivuko cha Azam Marine mara baada ya TEMESA kuingia makubaliano na Kampuni ya Azam Marine kutumia vivuko vya Azam Marine kufanya huduma katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2022 mara baada ya kuingia makubaliano na Kampuni ya Azam Marine kutumia vivuko vya Azam Marine kufanya huduma katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine Bw.Aboubakar Salim akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2022 mara baada ya kuingia makubaliano na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kutumia vivuko vya Azam Marine kufanya huduma katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2022 mara baada ya kushuhudia makubaliano kati ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) na Azam Marine kufanya huduma kupitia vivuko vya Azama Marine kwa wakazi wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya abiria wakiwa wakiingia kwenye kivuko kipya cha Azam Marine mara baada ya kuzinduliwa leo makubaliano na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kwaajili ya kufanya huduma hiyo katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Saalam. Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda kivuko kipya cha Azam Marine mara baada ya kuzinduliwa leo makubaliano na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kwaajili ya kufanya huduma hiyo katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Saalam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Wamezindua rasmi ushirikiano baina yao na Azam Marine ambao utawawezesha kutumia vivuko vya Azam Marine kwaajili ya kupunguza kero kwa wananchi wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wakiendelea kufanya ukarabati wa vivuko vyao.

Akizungumza baada ya kufanya makubaliano hayo leo Juni 13,2022 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala amesema wamekabidhiwa vivuko viwili ambavyo kila kimoja kinauwezo wa kubeba watu 250 kwa wakati mmoja hivyo basi kupitia vivuko hivyo vitaweza kufanya safari nyingi kwa siku kuliko vivuko vya kawaida kwani ni vivuko ambavyo vinatembea kwa haraka zaidi.

Amesema kuna gharama ambazo wamekubaliana na Azam wao kama TEMESA watalipa lakini kwa watumiaji wa huduma hiyo wataendelea kulipa gharama zilezile na wao kama TEMESA watajua ni namna gani wanaweza kumalizana na Azam.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine Bw.Aboubakar Salim amesema wameona kuna umuhimu mkubwa wa kuingia makubaliano na TEMESA kwasababu kumekuwa na changamoto ya vivuko kwa upande wa Magogoni na Kigamboni kupitia makubaliano hayo watawez kupunguza kero hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa ameipongeza Azam Marine kwa kukubali ushirikiano huo kwani watasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero ya vivuko kwenye eneo la Kigamboni.

Aidha amesema Serikali imekuwa ikiendelea kufanyia kazi changamoto moja baada ya nyingine ndo maana wakaamua kuingia makubaliano na Kampuni ya Azam Marine ikiwa ni moja wapo ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

"Serikali tayari imekwisha tenga fedha kwaajili ya kununua kivuko kikubwa zaidi ya Mv Magogoni ambayo itakuwa inauwezo wa kubeba abiria wengi zaidi pamoja na vyombo vingi vya usafiri kwa wakati mmoja". Amesema Mhe.Nyangasa.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: