PWANI.

BARAZA la Wakulima Taifa  (ACT) limepongeza bajeti ya Kilimo ya shilingi bilioni 750 itainua kilimo cha mboga mboga na matunda ambacho kwa sasa  kinaongoza kwa kusafirishwa nje ya nchi na kuliingizia Taifa pato kubwa.


Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Jitu Soni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kilimo cha matunda na mboga mboga kinaongoza kwa kuuzwa nje na ndani ya nchi na kinaliingizia taifa zaidi ya trilioni tisa.


Jitu amesema kuwa Mboga mboga na matunda yanaiingizia nchi fedha nyingi hata ukiunganisha mazao yote ya nafaka na mazao kama vile ya Korosho, mkonge, tumbaku na kahawa yote yakiunganishwa hayawezi kufikia mazao hayo ya mboga mboga na matunda kwani Aidha mauzo yake ya nje ya nchi  yana thamani ya  dola milioni 780 za Kimarekani kwa mwaka.


Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kibaha Hildelitha Msita alisema kuwa wanaendelea na utafiti wa mbegu za mazao ya miwa, mihigo na viazi na zimeanza kuzalishwa Kibaha.


Msita alisema kuwa wataweka mashamba mengi kwa baadhi ya wakulima ili yatumike kama mashamba darasa hivyo wanapoletewa elimu kwenye shamba wayatunze ili kuwasaidia na wakulima wanaozunguka ili mbegu zifike ngazi ya Vijiji na Kata.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: