Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga  na Waziri wa Uchumi wa Buluu Mhe. Suleiman Masoud Makame wakiskiliza malalamiko ya mwekezaji wa Hoteli ya Cheater iliyopo Shehia ya Kama Wilaya ya Magharib A Unguja, kuhusu kelele za wavuvi zinazopelekea kuamsha wanyama wakiwemo Simba, Chui na wanyama wengine wanaofugwa katika eneo hilo kwa ajili ya utalii pamoja na harufu za madagaa zinazozalisha wadudu wanaowaletea madhara kwa wanyama hao ikimo vidonda katika miili yao.

Maamuzi ya Serikali katika mkutano huo kwa  muekezaji wa Hotel hiyo ni kumtaka kutekeleza ahadi ya kuwajengea soko wavuvi na waanika madagaa kama makubaliano yalivyokuwa hapo awali wakati wa kuanza taratibu za uwekezaji wake huku wakimuomba kuendelea kustahamili uwepo wa harufu mbaya inayosababishwa na dagaa huku serikali ikiandaa mipango mizuri ya kuwajengea wavuvi hao maeneo ya kisasa ya kufanya shughuli zao 

Nao wananchi wametakiwa kupunguza baadhi ya tabia ambazo zinaleta changamoto za kuharibu baadhi ya shughuli za hoteli hiyo ikiwemo kupiga kelele zinazopelekea kuwaamsha wanyama wanaofugwa kwenye eneo hilo kabla ya wakati.

Aidha Serikali imeziomba pande zote mbili kujenga mashirikiano ya karibu  na kusaidiana katika mambo mbali mbali ili kujenga uhusiano mwema baina yao.



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: