Mwanza


Waandishi wa habari Mkoani Mwanza wametakiwa kuandika habari zitakazileta tija katika Jamii na kuacha kujiingiza kwenye mitego ya kuandika habari za upotishaji.


Rai hiyo umetolewa na Meneja wa TCRA Francis Mihayo Mkoani hapa wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoandaliwa na Shirika la internews kwa kushirikiana na USAID na yenye lengo la kuwakumbusha waandishi jukumu  la kusoma maadili ya uandishi wa habari na  sheria na taratibu kama zilivyoainishwa kwenye sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.


Mihayo ameleeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi kuhakikisha wanafanya kazi Kwa mjibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.


Amesema kuwa sekta ya habari zimezidi kupamba Moto hasa Kwa waandishi wa habari za mtandaoni kitendo ambacho hupelekea wengi kudumbukia kwenye mitego ya uandishi wa kupotosha hivyo ni lazima kuwaepusha waandishi kwenye dimbwi hilo.


Aidha ameleeza kuwa kumekuwa waandishi wa na wamiliki wa blogs wanapaswa  kuandika habari ambazo maudhui ya ndani na nje yyanaendana." Mimi kuna siku nilimpigia mwandishi mmoja baadae ya kuona alichokiandika kwenye blog yake kama kichwa cha habari hakiendani na nilichoka ndani akanijibu kuwa anatafuta watazamaji" alisema Mihayo.


Mihayo amesema kuwa baada ya serikali kufungulia Uhuru wa vyombo vya  habari waandishi waandishi wengine wanasajli TV zao na Blog Kwa gharama nafuu ya sh 500,000 baada ya kupewa usajili hivyo hupelekea kuweka habari zisizo sahihi.Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza   Edwin Soko amesema kuwa waandishi wanapokuwa kufanya kazi kwa kufata misingi ya kitaaluma na maudhui ya habari ya mwaka 2010 ya EPOCA ambayo inamtaka mwandishi kuzingatia miiko ya uandika.


"Tuna ramani kuona waandishi w habari wakifanya kazi zao Bola kuvunja sheria wala kukubwa kwenye mkondo WA sheria lakini Pia waweze kubaini habari zisizo sahihi na kuziepuka" alisema Soko.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: