Na John Walter-Babati

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 zimeweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Nakwa kata ya Bagara, Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara  kwa kiwango cha lami nyepesi urefu wa kilomita 1.6 yenye thamani ya shilingi Milioni 999,550,0,000.
Kukamilka kwa barabara hiyo itarahisisha zaidi mawasiliano kipindi chote cha mwaka hasa wakati wa mvua ambapo ilikuwa inaleta usumbufu kwa wananchi.
Mpaka kufikia juni mwaka 2022 mji wa Babati una bara bara za lami kilomita 11.94.
Mradi huo unatekelezwa na serikali kupitia wakala wa bara bara (TARURA) kwa fedha za mfuko wa jimbo shilingi milioni 499,550,000.00, gharama za tozo ya mafuta shilingi Milioni 500,000,000 na upo chini ya  mkandarasi M/s Ravji Construction Ltd.
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema mradi huo utakapokamilika wananchi watafanya shuguli zao za kijamii bila usumbufu katika majira yote ya mwaka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kuelekeza fedha ziende kwenye miradi mbalimbali na kwamba ataendelea kuwasemea wananchi wa Jimbo lake ili changamoto zinazowakabili zitatuliwe kwa wakati.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2022 "Sensa ni msingi wa mpango na maendeleo; Shiriki kuhesabiwa,tuyafikie maendeleo ya Mwenge ya Taifa".
Share To:

Post A Comment: