WAKAZI zaidi ya 1,600 katika Kijiji Cha Mkoko ,kata ya Msata , Bagamoyo Mkoani Pwani wanakwenda kuondokana na kero ya kunywa maji machafu yasiyo salama kiafya pamoja na kuliwa na mamba katika mto Wami ,baada ya Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA )kukamilisha Mradi wa maji Mkoko .


Kero hiyo ni ya muda mrefu hali iliyosababisha baadhi ya watu kujeruhiwa na wengine kuliwa na mamba wakati wakifuata maji kwenye mto huo.

Akizindua mradi wa maji kijiji cha Mkoko na kitongoji cha Mtoni pamoja na kutembelea ujenzi wa mradi wa maji Fukayose uliowekwa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru 2022 na kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuikabidhi DAWASA kuendelea na hatua ya uendeshaji wa miradi hiyo ,mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah aliridhishwa na miradi hiyo na kupongeza mahusiano mazuri ya Taasisi hizo.

Alisema RUWASA imepokea fedha za Uviko19 kutekeleza miradi nane kati ya hiyo ni mradi wa Mkoko ambao mkandarasi Lukedan Contractor amemaliza ujenzi kabla ya muda .

"Rais Samia Suluhu Hassan anaupiga mwingi, na Ni Kama jina lake Suluhu ,amekuwa Suluhu wa kero za wananchi nchini , tumeshuhudia ametoa fedha nyingi za Uviko19 kujenga miradi ya miundombinu ya madarasa na miradi ya maji na Sasa inaleta matokeo chanya"

"Kwa spidi ya Rais ,pia tunahitaji wakandarasi wa aina hii ,nampongeza mkandarasi Lukedan kwani amekamilisha ujenzi kabla mwezi mmoja wa mkataba wake "alisema Zainab.

Zainab alieleza, mradi huu umeenda kwenye vituo Tisa,ameitaka Ruwasa kuhakikisha wanamtua mwanamama ndooo kichwani kwa kupanua mradi ili ufike majumbani.

Alitoa Rai kwa wananchi kuulinda na kutunza miundombinu ya maji ili isiharibike kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Nae James Kionaumela alifafanua, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia fedha za Uviko19 ilianza utekelezaji wa mradi huo ,chanzo chake cha maji kutoka Bomba kuu la DAWASA ,ukihusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 50,000 juu ya ardhi, ujenzi wa vituo tisa vya kuchotea maji ambapo umegharimu milioni 348.4.

Kuhusu mradi wa Fukayose umetekelezwa kwa fedha za Uviko19 kwa gharama Zaidi ya milioni 350 ambapo ujenzi umefikia asilimia 95 , wanatarajia kaya 374 kupata huduma ya maji na Lengo ni kusaidia wananchi 2,242 ambao huduma haijawafikia ikiwemo vitongoji vya Umasaini na Lusako.

Kionaumela pia alielezea utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji kitongoji Mtoni Bagamoyo, Lengo kusaidia wananchi 1,169 .

Alisema ulitekelezwa mwaka wa fedha 2020/2021 kupitia fedha za mfuko wa maji (NWF) ambao chanzo ni maji kutoka Bomba kuu la DAWASA Ukihusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 50,000 juu ya mnara wa 12m na ujenzi wa vituo kumi vya kuchotea maji kwa gharama ya milioni 181.4 kwa kutumia wataalamu wa ndani (Force account).

Baadhi ya Wakazi akiwemo Huruka na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mkoko ,Mtoro Masimba walisema walikuwa wakipata shida ya maji kwa kuyapata mtoni ambapo walikuwa wakiliwa na mamba.

Jumanne Mavulla ni majeruhi wa kuliwa mkono wake wa kulia na mamba ambae ameshukuru mungu kupona na kudai ,Rais Samia kawatendea haki na kupatiwa huduma ya maji safi na salama.

Nae mhandisi Danny Isaac Amata , mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya LUKEDAN ambao ndio wajenzi wa mradi huo anaishukuru serikali ":;kwa fursa hii Kama mkandarasi wa ndani, hii ni kwa maana ya Serikali kuu na wizara ya maji kupitia RUWASA mkoa wa Pwani, maana sisi kama wakandarasi kupata kazi ni fursa ya kuonesha uwezo na kuhudumia wananchi.
Share To:

Post A Comment: