Na,Jusline Marco;Arusha


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Ackson mgeni rasmi katika mkutano wa wabunge wa kikanda kwenye Bunge la Afrika Mashariki unaofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo leo jijini Arusha.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanawake wa Bunge la Afrika Mashariki EALA kutoka Nchini Rwanda Mhe.Fatma Ndangiza amesema mkutano huo
umelenga kubadilishana uzoefu na mawazo kwa wanawake walio katika ngazi za siasa.

Mhe.Fatma amesema kwa ushirikiano na Shirika la kimataifa linalo jishughulisha na masuala ya demokrasia na maendeleo ya wanawake IDEA wameandaa mkutano huo wa Wabunge wa Kikanda ambao utahusisha Jumuiya mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya SADC pamoja na Jumuiya ya Afrika Magharibi.

Aidha amesema kauli mbiu katika mkutano huo imelenga kubadilishana uzoefu kwa mchango wa wanawake katika siasa,changamoto zinazowakumba  na mafanikio ili waweze kusaidia wanawake na vijana kwa kupaza sauti ya mwanamke na kuweza kuchaguwa kuwa viongozi.


Kwa upande wake Msemajibwa Wabunge wanawake katika bunge hilo Mhe.Pamela Maasai amesema kuwa mkutano huo umelenga kuwaleta wabunge wanawake pamoja kutoka maeneo mbalimbali ya Jimuiya za Kikanda kuweka mitazamo ya pamoja itakayoleta matokeo chanya ndani na nje ya Jumuiya.




Share To:

JUSLINE

Post A Comment: