Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji wa Bunge la Afrika Mashariki Christopher Nduwayo akiongea na waandishi wa habàri kwenye Makao Makuu ya Bunge Wakati wa kikao Cha 15 Cha Bunge la EALA

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki EALA Dkt. Abdullah Makame akiongea na waandishi wa habàri Wakati wa mjadala wa kuchangia mjadala wa Kamati ya Mawasiliano uliowasilishwa Jana picha zote na Ahmed Mahmoud


Na Ahmed Mahmoud


Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji wa bunge la Afrika Mashariki EALA  Christopher Nduwayo amezitaka nchi za Jumuiya hiyo kuzisisitiza Idara za uhamiaji za nchi zao kufuata sheria ya Jumuiya inayoelekeza suala utoaji wa viza.


Akiwasilisha Taarifa ya kamati hiyo mbele ya Bunge hilo alisema kuwa ipo haja kubwa ya kuangalia suala zima la utoaji wa viza hususani kwa wananchi kutoka nchi za Jumuiya hiyo.


Alisema kumekuwepo na changamoto ya Maafisi uhamiaji katika maeneo ya mipaka kuendelea kutoa viza ya siku Saba wengine mwezi ambapo ni kinyume na utaratibu wa sheria ilipitishwa na nchi hizo.


"Unakuta Mwananchi anatoka Burundi anapewa viza ya siku Saba na Mwananchi huyo mfano anaenda nchi Tanzania Jijini Dar es Salaam kufika huko lazima atumie siku mbili za kwenda hapo anabakiza siku tano kufanya biashara kwa siku hizo hadi kurudi mpakani ni siku chache inayopelekea akifaka mpakani kulipa faini hii ni usumbufu kwa Mwananchi"


Amebainisha kwamba ni vyema kila nchi ikafuata utaratibu wa sheria ulipitishwa na nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuwapa viza ya miezi sita kila mwananchi anayetaka kusafiri ili kupunguza usumbufu unaoendelea kujitokeza katika mipaka na kuwatia hofu ya kufanyabiashra.

"Jumuiya yetu imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia na kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa Wafanyabishara wanaozunguka katika kufanya biashara zao eneo Moja la nchi Moja hadi nyingine kupitia mipaka ya nchi za Jumuiya" Alisema Nduwayo.

Alisema kwa ipo haja ya kuangalia pia suala zima la vibali vya kazi ambapo wafanyakazi wa kazi ndogondogo Jumuiya iliafiki waruhusiwe kufanyakazi lakini bado wamekuwa wakipata vikwazo mbalimbali wanapovuka mipaka ya nchi zetu.

"Mfano Mimi ni mbunge nilipita katika Moja ya mpaka wakanigongea kibali Cha mwezi Moja tena baada ya kuuliza kihusiana na sheria hiyo ya miezi sita na bado katika Passipoti yangu waliniandikia kitofanyakazi popote Sasa nashangaa Mimi ni Mbunge na huku nakuja kufanyakazi ya kuwatumikia wananchi wa Jumuiya ni vyema serikali zetu zikaa na kutoa Elimu ya kutosha kwa maafisa Hawa wa Uhamiaji hususani katika mipaka yetu"


Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame alisema kwamba baadhi ya mipaka katika vituo vya mipakani hakuna makazi ya watumishi wakiwemo Uhamiaji TRA na Polisi ambapo inapelekea wafanyakazi wa Idara hizo kufanyashighuli zao bila ufanisi.

Alisema Kutokana na hilo ni vyema kila nchi itengeneze utaratibu wa kuwajengea nyumba au makazi yenye viwango watumishi wao kwenye vituo hivyo ili wafanyekazi kwa ubora na ufanisi mkubwa.

" Aidha katika kipaumbele alichopanga Katibu Mkuu  wa Jumuiya hiyo alipoingia katika nafasi yake alipanga kazi yà kwanza ni kuongeza mwanachama mpya Jambo ambalo amelitekeleza kwa kumpata DRC CONGO ambayo inamalizia utaratibu ili kuingia rasmi baada ya hilo kazi nyingine kubwa aliopanga ni kuunda kamati ya biashara ya Afrika Mashariki ili kuokoa watu wa sekta binafsi"

Aliongeza kuwa atatumia nguvu kuhakikisha kwa Mwaka huu kamati hiyo inapatikana ili kupunguza tatizo la Kodi mipakani pamoja na changamoto zake. 

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: