Naibu Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Christopher Timbuka akizungumza kwenye kikao Maalimu na Waandishi wa Habari kilichofanyika jijini Arusha tarehe 29 Juni, 2022,akieleza kuhusu taarifa zilizoripotiwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna Ng’ombe wamekufa baada ya kuhamia Kijiji cha Msomera ambazo hazina ukweli na kueleza kuwa picha hizo ni za Ng’ombe waliokufa katika nchi ya Jirani kutokana na matatizo ya ukame mwaka 2018.

 MKURUGENZI wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Maurus Msuha ameelezea hatua kwa hatua kuhusu historia ya Hifadhi ya Ngorongoro huku akitumia nafasi hiyo kuuliza maswali ya msingi ambayo wananchi wa kada mbalimbali wanapaswa kujiuliza kuhuse eneo hilo.


Akizungumza sehemu ya historia ya eneo hilo alipokuwa akitoa wasilisho mbele ya wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari Mkurugenzi wa Wanyamapori … sote wanafahamu hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1959 na ilikuwa na malengo makuu matatu.

Amesema jambo la kwanza ni uhifadhi ,suala la pili kuendeleza jamii inayoishi katika maeneo hayo na jambo la tatu kuendeleza utalii na kwamba ukisoma nyaraka mbalimbali unaweza kusema hiyo ilikuwa kama majaribio kuweza kuona inawezekana, kwasababu katika hali ya kawaida unajaribu kuangalia masuala matatu muhimu kutokea katika eneo moja, uhifadhi, maendeleo katika jamii na utalii.

“Kwa wakati huo nadhani waliona pengine inawezekana , lakini kuna jambo moja ujue Ngorongoro ilikuwa sehemu ya Serengeti kabla ya Serengeti haijawa hifadhi ya taifa , na wakati Ngorongoro inaanzishwa kuna wananchi takribani 4000 walihamishwa kutoka Serengeti ili Serengeti sasa iwe ni hifadhi ya taifa.

“Kwasababu kwa mujibu wa sheria ikishakuwa hifadhi ya taifa makazi ya watu hayaruhusiwi, kwa hiyo wananchi sasa wakatolewa kule ambao walikuwa wanakadiriwa takribani wananchi 4000 wakaletwa Ngorongoro ambako nako kunakadiriwa kulikuwa na watu 4000 kwa wakati huo.

“Hivyo wakati inaanzishwa mwaka 1959 inakadiriwa kulikuwa na watu takribani 8000 .Ngorongoro ina makabila matatu na hili naomba niliseme kwasababu kwa bahati mbaya halisemwi sana , sijui ni kwasaabu ipi , ukweli unapoongelea wenyeji wa Ngorongoro unaongelea makabila matatu na sio Wamasai yake tu kama watu wamekuwa wakisema na haya ndio makabila ya wamasai.

“Nitawaambia kila mmoja alifika lini Ngorongoro ,Wahazabe waliingia Ngorongoro zaidi ya miaka 3000 iliyopita, wao ndio walikuwa wa kwanza , na mpaka leo wapo ,Wadatoga miaka 400 iliyopita , Wamsai wameingia Ngorongoro miaka 250 iliyopita lakini ukichukulia wingi wa watu Wamasai ndio wengi zaidi kuliko haya makabila mengine,amesema.

Amefafanua “Nimeamua kueleza haya kwasababu gani unaposema kwamba watu wanahama kwa hiyari kama nitakavyokuja kusema baadae tusiseme Wamasai wanahamishwa kwa hiyari, wanaohama kutoka Ngorongoro ni haya makabila matatu maana ndio wakazi wa maeneo haya .

“Na wanahama kwa hiyari, nini umuhimu wa hili eneo ,hili”Eneo ni muhimu sana kwa maana ya uhifadhi na maendeleo ya utalii na sote tunafahamu tunapoongelea utalii tunaongelea ajira, upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo yetu.”

Ameongeza eneo hilo mwaka 1979 lilitambulika kuwa eneo la Urithi wa Dunia na kulikuwa na sababu mbalimbali ambazo zilifanya liwe urithi wa dunia.Miongoni mwa sababu hizo kwanza kulikuwa na wanyama wengi wanahama ikiwemo Punda milia na Nyumbu kwa upande wa Loliondo.

“Lakini idadi kubwa ya aina ya wanyamapori walikuwa wanapatikana eneo hilo ni wengi sana unaongelea aina 119 lakini uwepo wa wanyama wale ambao wapo katika hatari ya kutoweka kwa mfano Vifaru na Mbwa mwitu.Ukienda Creta wingi wa wanyama wale , idadi ya ndege katika eneo hilo.

“Kwa wakati huo wa mwaka 1979 UNESCO ilipoona sifa hizi zote imeitambua Ngorongoro kama eneo la urithi wa dunia.Lakini mwaka 2010 Ngorongoro ikaonekana ina sifa nyingine kwa maana ya sio zile tu za kiuhifadhi lakini ina masuala mengi yanayohusiana na tamaduni , historia ya mwanadamu.

“Na ndio eneo pekee lenye historia iliyokamilika ya mwanadamu kuanza kutembea akiwa amesimama , eneo ambalo tumeona hizi nyayo,eneo ambalo kuna historia ya Old Vai na inaonesha mabadiliko ya binadamu.Kutokana na sifa hizi na zile za mwanzo ikapewa sifa nyingine ya pili .

“Hili ni eneo la urithi mchanganyiko ile ya kwanza na hii ya pili, pia kuna kijilojia, mifumo ya miamba umeonesha kuwa wa kipee sana , kwa hiyo mwaka 2018 eneo hili lilipewa sifa nyinge na UNESCO kwa kulitambua kwa sifa tatu. Lakini kumekuwepo na mafanikio katika hii miaka 63 tangu Ngorongoro ianzishwe,”amesema Dk.Msuha .

Ametaja kuwa moja kama alivyoeleza lakini kuunganisha hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti nayo ikafanya iwe na sifa nyingine na mwaka 2013 ilipewa sifa nyingine kuwa ni moja kati yale maajabu saba ya dunia.

“Lakini jingine limekuwa la mafanikio ni kuongezeka kwa wanyama ambao ni muhimu na hii nazungumzia hasa hasa Faru kwa mfano idadi yao imekuwa ikiongezeka na imekuwa ikiimarika lakini suala zima la udhibiti wa ujangili haya ni mafanikio ukiondoa eneo la mapato na mengine.

“Sasa pamoja na umuhimu huu wote ambao tumeuona katika eneo la Ngorongoro eneo hili lina changamoto nyingi , moja kati ya changamoto uanzishwaji wake ulilenga katika kuwa na uwiano wa mambo matatu , uhifadhi, maendeleo ya jamii na utalii.

“Sasa unaipate hii mizania iweze kukaa sawa , hiyo imekuwa changamoto, moja ya mambo ambayo tunaona katika kipindi hiki chote ni kwamba idadi ya watu imeongezeka, nimesema wakati inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa takriban watu 8000 lakini kwa sasa tunaongela idadi ya watu imefika zaidi ya 100,000 ambayo ni mara 10 zaidi ya wakati ilivyokuwa imeanza.Sote tunaona na nyie ni mashahidi ongezeko la makazi katika eneo hili.

“Kuna ongezeko la mimea vamizi lakini baadhi ya hawa wanyamapori wamepotea kabisa , kuna ongezeko la mifugo kutoka 260,000 mpaka inafikia milioni moja , sasa shughuli zote hizi kama makazi yanaongezeka , mifugo inaongezeka, mimea vamizi inaongezeka , hebu jaribu kufikiri ule uwiano sasa wa kuhifadhi , maendeleo ya jamii na utalii unaupataje katika mazingira kama haya,”amesema.

Ameongeza Je makazi yanapoongezekana haipunguzi eneo la malisho na wanyamapori, je muingiliano wa wanyamapori na wananchi hauongezeki, kwa hiyo kuwa na mambo mengi , changamoto hizo zinazojitokeza lakini kwa upande mwingine kuna maswali tunapaswa kujiuliza.

“Kwanini umasikini uongezeke ?Tunasema idadi ya mifugo inaongezeka inakuaje watu ambao mifugo ndio njia kuu ya uchumi wakuwa masikini?Mifugo inaongezeka uchumi unaongezeka nini kinachotokea katikatika yao umasikini unaendelea kuwa mkubwa.

“Lakini suala la elimu , idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ni kubwa sana ukilinganisha na maeneo mengine, haya yanatokea kwenye eneo ambalo kuna shule 25 za msingi , kuna shule mbili za sekondari, sasa kwanini eneo ambalo lina shule bado watu wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 64?

“Nini kinachoendelea katika eneo hili, hayo ndio maswali ya kujiuliza , haiwezekani kila kijiji kina shule , kuna sekondari halafu asilimia 64 haijui kusoma na kuandika , hizi shule zilijengwa kwa ajili ya nini?Kuna nini nyuma ya pazia , muingiliano na ongezeko hili la idadi ya watu kutakuwa na muingiliano wa magonjwa kwa maana ya magonjwa yanayotoka kwenye mifugo, wanyama pori na binadamu.

“Kutokana na huu muingiliano kuna magonjwa mengine utayakuta kwa binadamu, utayakuta kwa wanyamapori , utayakuta kwenye mifugo , sasa hiyo nayo ni changamoto,”amesema Dk.Msuha wakati akielezea kuhusu historia ya eneo hilo la Ngorongoro.

Ametumia nafasi hiyo pia kuelezea matukio mbalimbali ya vifo yaliyotokana na wanyapori kuu binadamy kwenye eneo hilo akitolea mfano mtoto kuliwa na samba wakati akitoka shuleni huku mwingine akishuhudia tukio hilo baada ya kufanikiwa kupanda juu ya miti.

“Hivyo kuna changamoto na hivyo Serikali ilifanya utafiti kwa kushirikisha wadau kwa ngazi tofauti , wakajiuliza nini kifanyike? Wananchi wanaoishi Ngorongoro walikuja na maoni yao na moja walisema wanaona watanzania wenzao wanajenga nyumba.

“Hivyo na wao wangependa kuona wanapata maendeleo kama watanzania wengine na hilo ni dai hahali,Swali ni je aina hiyo ya maendeleo yanapatikana katika eneo hilo?Pia walisema wanataka kupata manufaa zaidi, wanahitaji kumiliki ardhi, swali linakuja unawezaje kumiliki ardhi katia eneo ambalo limehifadhiwa?

“Unaposema unamilikishwa ardhi kwenye hifadhi hii ni changamoto na mimi nasema hili ni dai la msingi na kila mmoja wetu anaweza kuwa na kipande cha ardhi lakini wakazi wa Ngorongoro? Lakini wanahitaji kulima, kupanda mazao na hili lilikuwa dai muhimu

“Lakini linaweza kufanyika ndani ya msingi.Haya ni maswali ya kujiiliza , kwa maana ya madai ni madai ya msingi.Yote ambayo tunahitaji huku nje na wenzetu wa Ngorongoro walikuwa wanahitaji na hapo ndipo Serikali ikaona kuna haja ya kuangalia namna ya kutekeleza madai hayo, na changamoto inakuja haya mambo unaweza kufanya ndani ya hifadhi?”Alihoji.

Aidha amesema kuwa mchakato wa kufanya utafiti umefanyika kwa miaka miwili na walirekodi kuhusu majadiliano yaliyofanyika katika vijiji vyote 25 .Kua maoni mengi yalitolewa yakiwemo ya kupanua eneo la Ngorongoro ili kuwa kubwa zaidi lakini swali la msingi ukifanya hivyo unatatua tatizo au unahairisha kwa muda tu.

“Wengine wakasema labda Ngorongoro ibadilishwe labda liwe pori la akiba.Ukisema utapunguza watu na mifugo lakini ukweli ni kwamba idadi itakuja kuongezeka,”amesema Dk.Msuha alipokuwa akielezea kuhusu hifadhi ya Ngorongoro na hatua mbalimbali za majadiliano ambazo zimefanyika kabla ya wakazi kuanza kuhama kwa hiyari eneo hilo.


Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Tanzania Dkt. Maurus Msuha akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu zoezi la uwekaji wa alama katika pori tengefu la Loliondo na zoezi la Wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga,kwenye kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika jijini Arusha tarehe 29 Juni, 2022.



 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa kwenye mkutano huo maalumu.

 





 
Share To:

Post A Comment: