Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwasili Bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 05 Mei,2025 akiwasilisha Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mpango na makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.
Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Mhe. Abdallah Ulega ameliambia Bunge la Tanzania kuwa serikali ya awamu ya sita inaendelea na taratibu za kutunga sheria ya Majengo itakayokuwa na jukumu la kusimamia sekta ya majengo nchini, ili kutumika kama mwarobaini wa changamoto zilizopo hususan katika masuala ya uratibu, usimamizi na udhibiti wa sekta ya majengo nchini.
Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo Leo Jumatatu Mei 2024, Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka 2025/26, akieleza kuwa kutungwa kwa sheria hiyo ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kutokea kwa ajali ya kuporomoka kwa Jengo la ghorofa nne katika eneo la Kariakoo Jijini Dar E salaam, mnamo Novemba 16, mwaka 2024 na kusababisha vifo, majeruhi pamoja na upotevu wa mali.
"Nitumie fursa hii kutoa pe kwa wote walioathirika kwa namna moja ama nyingine na maafa haya na ninawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani" amesema Waziri ulega.
Katika hatua nyingine Waziri Ulega amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuliongoza Taifa, akisema watanzania wote ni mashuhuda wa namna alivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta zote nchini, akieleza kuwa chini ya Uongozi wake miradi mikubwa imetekelezwa, suala ambalo litasaidia kuchochea maendeleo katika sekta nyingine za kiuchumi na kijamii na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Post A Comment: