Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Grace Magembe  amewashukuru wananchi kwa kuwa wazalendo kwa  kuchangia nguvu kazi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini .


Amewataka kuendeleza ari hiyo kwa kuendelea   kushirikiana na Serikali katika   kuleta maendeleo nchini, akisisitiza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi  unapunguza gharama za ujenzi,unatoa ajira kwa vijana , unaimarisha   usimamizi , ulinzi na kuwafanya wananchi wamiliki wa miradi hii.


Hayo yamebainishwa  tarehe 27 Juni 2022 katika ziara ya Dkt. Magembe alipokuwa anakagua ujenzi wa miundombinu pamoja utoaji wa huduma katika Kituo cha afya Rubare kilichopo Halmashauri ya Wilaya Bukoba  Mkoani Kagera.


“Kupitia kituo hiki cha Rubare  nitoe  shukrani kwa wananchi wote ambao wameshirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.


Serikali inathamini mchango wa nguvu kazi,usimamizi kupitia kamati mbalimbali mlizounda,utoaji wa maeneo ya ujenzi na mengineyo mmethibitisha kuwa maenedeo yetu watanzania yanaletwa na sisi  wenyewe" Dkt. Magembe


Aidha  Dkt. Magembe hakuridhishwa na utekelezaji  wa ujenzi Kituo cha Afya Kashai kilichopo Manispaa ya Bukoba ambacho kipo nyuma ya utekelezeaji kwa miezi 6, amemuelekeza Mkurugenzi kuwasilisha maelezo  ya kilichopelekea ucheleweshwaji huo sambamba na mpango kazi wa ukamilishaji wa mradi huo  kwa  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Share To:

Post A Comment: