Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua
kikao cha 17 cha maafisa habari, mawasiliano na Uhusiano wa Serikalini kinachoketi kwa siku tano jijini Tanga
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua
kikao cha 17 cha maafisa habari, mawasiliano na Uhusiano wa Serikalini kinachoketi kwa siku tano jijini Tanga
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Dkt Jim Yonaz akizungumza wakati wa kikao hicho

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa. Habari na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa kikao
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa. Habari na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa kikao
Sehemu ya Maafisa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri Nape
Sehemu ya Washiriki kwenye kikao hicho


NA OSCAR ASSENGA, TANGA

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameagiza utengenezwe utaratibu wa mafunzo kwa Maafisa Habari nchini juu ya miradi mikubwa ya Kitaifa inayotekelezwa na serikali ili wawe na uelewa wa kuisemea miradi hiyo wakati wowote. 

 Aliyasema hayo leo wakati  alipokuwa akifungua kikao cha 17 cha maafisa habari, mawasiliano na Uhusiano wa Serikalini kinachoketi kwa siku tano jijini Tanga ambapo alisema lazima maafisa habari hao wawe wanajua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili kuweza kujua namna ya kuielezea kwa wananchi.

 Alisema wote wanafahamu katika mwaka mmoja wa Rais Samia ameleta mageuzi makubwa yaliyofanyika hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kila afisa habari hata anapoamshwa usingizini awe anaijua mambo yanayoendelea akiamini wakifanya hivyo watawapa uwezo wa kitu cha kueleza.

 

Aidha alisema hivyo kutokana na hayo ni lazima maafisa habari waliopo kwenye maeneo ya mikoa husika wachukue muda wa kuelewa miradi inayoendelea kwenye maeneo yao ili wawe kuwa na jambo la kusema akitolea mfano Mkoa wa Tanga ujenzi unaoendelea wa kuwahamisha watu wanaotoka Ngorongoro kuja Msomera wilayani Handeni  hivyo Afisa habari wa Tanga na maeneo yale wanapaswa kufahamu kwa kina kinachoendelea. 

 

Hata hivyo Waziri Nape aliagiza uandaliwa mjadala ya maafida wa habari kwa kutumia te teknolojia ya kisasa ili kupunguza gharama kubwa  kwa kufanya majadiliano ya pamoja kupitia teknolojia jambo ambalo amesema linawezekana. 

 

Waziri Nape pia alitoa siku 14 kwa Maafisa habari nchini kuhakikisha kila tovuti ya serikali  iwe na taarifa zinazoendana na wakati huku akiahidi kuwashughulikia watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo. 

 

Pia  amewataka maafisa habari wa serikali wasiruhusu watu wapotoshe mafanikio ya serikali na badala yake wametakiwa kujibu hoja ili kuwaelewesha wananchi. 

 

Alisema kwani kumekuwa na tatizo sugu la muda mrefu katika tovuti na mitandao ya kijamii za Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali kuwa na habari zilizopitwa na wakati. 

 "Nitoe siku 14 kuanzia tarehe 14 Mei kila tovuti ya serikali au taasisi ya serikali au serikali za mitaa iwe na taarifa zinazoendana na wakati afisa habari atakayeshindwa kutekeleza hili ndugu Msigwa hatutaweza kuendelea naye inabidi tuachane naye, "Alisema Waziri Nape. 

Alisema anajisikia vibaya sana anapopita na kusikia  kuna taasisi za serikali tovuti za Mkoa za wizara,  Wilaya au Halmashauri zina taarifa za miaka miwili au mitatu  iliyopita halafu tuna afisa habari kwenye hilo eneo haiwezekani jamani na tusipoambiana tutakuwa hatutendeani haki jamani sasa siku 14 zinatosha kabisa Msigwa ulikague na nipate taarifa ya jambo hili. 

 Aliongeza kuwa nasikitika kuona tovuti ya wilaya,  Mkoa,  Halmashauri haziendani na wakati watu wengi wameacha kutembelea tovuti za serikali kwa ajili ya kuwepo taarifa zilizopitwa na wakati umefika sasa tutoke kwenye aibu hiyo imewafanya watu hawatembelei tovuti za serikali wakati kuna maafisa habari.

 "Mhakikishe mnajibu hoja za wananchi kwenye vyombo vya habari kwa wakati muafaka kuhusu changamoto zinazojitokeza msiruhusu watu wapotoshe ukweli kwani ukweli unapopotoshwa ni aibu kwa maafisa habari supu inanywewa ya moto usisubiri mpaka usukumwe kwenda kukanusha habari ambayo ni ya uongo akikibu saa moja saa mbili nawe sema tukiends hivyo watakuwa na nidhamu kwenye kupotosha, "alisistiza Waziri Nape.

Katika hatua nyingine Waziri Nape ameahidi kupeleka mara moja maafisa habari katika Mikoa 7 inayokabiliwa na ukosefu wa maafisa habari ikiwemo Mikoa ya Manyara, Lindi, Mbeya,Tabora,  pamoja na mikoa ya Kigoma,  Dodoma na Geita ambayo maafisa habari wske wamekuwa wasaidizi wa wakuu wa mikoa. 

Awali akizungumza katika kikao hicho ,Katibu mkuu wa wizara ya habari Jimmy Yonazi amesema tansinia ya mawasiliano kwa umma ni ya zamani na ni muhimu kwasababu ndio imeandika historia ya serikali juu ya namna inavyohudumia wananchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo. 

 Katibu mkuu huyo alimshukuru Rais Samia kwa kuifanya sekta hiyo kuwa pamoja na kupelekea kuwezesha taarifa kuwafikia wananchi jambo hilo linatoa taswira mpya lakini kutoa msukumo mpya na muelekeo mpya kwa  maendeleo nchini. 

 Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha katibu Mkuu ,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema kuwa ni heshima kubwa aliyopewa na Rais na hivyo wana deni kubwa la kulipa kwa kufanya kazi bila kuchoka usiku na mchana kwa kuzingaia uadilifu,  ubunifu,  na mabadiliko yanayotokes kila uchwao katika sekta hiyo nchini. 

 

"Tokea nimeteuliwa na mheshimiwa Rais kuwa Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo nimshukuru Mheshimiwa Waziri na katibu mkuu kwa kuwa wameweza kunishika mkono na kuniwezesha kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi bila vikwazo vyovyote, "alisistiza Msigwa. 

 

Mwenyekiti wa maafisa habari Nchini Pascal Shelutete alimshukuru waziri kwa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho huku akiahidi wao kama maafisa habari wa serikali hotuba ya Waziri ni maelekezo hivyo katika siku 5 watakazokuwepo jijini Tanga watahakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya kuyafanyia kazi maelekezo yote. 

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: