Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana Mei 25, 2022 amepokea mapendekezo kutoka kwa wananchi wa Tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.

 

Maoni hayo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu na wawakilishi wa wakazi wa wilaya hiyo wakiwemo Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Shangai, Malaigwanani, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana, ofisini kwake Mlimwa, Dodoma.

 

Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao kwani haiwezi kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake. “Msisikilize maneno maneno ya watu wa pembeni.”

 

Akizungumzia kuhusu eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni, Tanga ambako yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari alisema ujenzi unandelea vizuri.

 

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na pia, Serikali imepanga kuongeza nyumba nyingine lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa alisema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wote nchini wanapata tija kupitia shughuli hiyo.

 

 

 

 

Share To:

Post A Comment: