Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku tatu la Uhuru la vyombo vya habari linaloqnza Leo Jijini Arusha 1/5/2022-3/5/2022 likiwa na Kauli mbiu isemayo Uandishi wa Habari na changamoto za Kijiditi.
 Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti TEFF Bakari Machumu Akiwa katika kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari duniani Jijini Arusha.

 Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Gerson Msigwa akizungumza katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani lililianza Leo tar 1/5/2022 Jijini Arusha

 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Deodatus Balile akizungumza katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani lililianza Leo tar 1/5/2022 Jijini Arusha
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya habari kusini kwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) Salome Kitomari akizungumza katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani lililianza Leo tar 1/5/2022 Jijini Arusha

 Viongozi wa Wakijadili jambo kabla ya mjadala kuanza katika akizungumza katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani lililianza Leo tar 1/5/2022 Jijini Arusha.Na.Vero Ignatus,Arusha


Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutokukubali kutumika kwa manufaa ya watu Fulani badala yake wawe kwenye misingi yenye weledi wa uandishi wa habari ili waweze kupata heshima katika Jamii kutokana na kazi wanayoifaya.

Hayo yamesemwa na Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Gerson Msigwa katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani lililianza Leo tar 1/5/2022 nchi zote duniani na kwamba sekta ya habari inategemewa, hivyo maadili na uadilifu unahitajika katika utendaji kazi

Msigwa amesema kuwa Sekta ya habari ni sekta ya uwekezaji Kama ilivyo sekta nyingine,hivyo maadili yasipozingatiwa itatokea migongano wa maslahi hivyo ni jukumu la waandishi kuangalia ni namna ya kuilinda taaluma hiyo

Amesema kuwa ili wanahabari waweze kuwa imara lazima waangalie changamoto ambazo zinazotokana na wao wenyewe na kuzitatua.

" Waandishi kutumika kwa wadau na siyo taaluma,Unakwenda kuandika habari ambayo tunajua kabisa huyu katumwa na mtu Fulani kwa masilai yake ukifika hapo watu ambao wapo kinyume na hayo matwakwa lazima mtaingia kwenye mgongano"

"Waandishi wa habari tukubaliane tunatumika mnoo,sio kwenye uchaguzi,kwenye biashara za watu,kwenye milengo mbalimbali ni kitu kinashusha hadhi Sana na kinatuvunjia Sana heshima kwa jamiii”alisema Msigwa

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya habari kusini kwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) Salome Kitomari amesema kuwa wanasherehekea siku muhimu kukiwa na changamoto kubwa ikiwemo hali duni ya uchumi wa wanahabari kwa maslahi na maisha jambo ambalo halijakaa sawa

Kitomari amesema Kumekuwa na kunakili sheria mbalimbali ambazo zinamkandamiza Mwandishi Sambamba na ukuaji wa teknolojia ,mitandao ya kijamii,pamoja na yanapoteza maudhui na Jamii,jambo ambalo wanapaswa kuweka mikakati ya kuitatua.

"Mwandishi lazima abadilike,aende na wakati pamoja na kuzingatia weledi maudhui ya taaluma ili kujenga Imani kwa wananchi"alisema kitomari

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa TBC Taifa Dr.Ayubu Ryoba amesema kuwa uhuru wa vyombo vya habari unapiganiwa yangu mwaka 1993 ambapo mambo mengi chanya yametokea ,ukiwemo ukuaji wa teknolojia wa habari za mtandaoni jinsi ulivyobadilisha utendaji kazi wa uandishi wa habari.

"Haya mambo ya kidigital yamefanya kila mtu kuwa Mwandishi wa Habari japokuwa hawawi na weledi hivyo matendo yetu tunayoyafanya Jamii inayaona"

Amesema wapo watu wanaotumia vibaya mitandao hiyo ya kijamii kwa kuvunja Amani ya nchi na kwamba ifike mahali mitandao hiyo idhibitiwe kwa kuangalia namna gani Bora wataweza kuitumia kwa manufaa zaidi
Share To:

Post A Comment: