Zaidi ya Wanafunzi 15 wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wanashiriki maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolonia na Ubunifu ( MAKISATU) yanayofanyika mkoani Dodoma.

Mmoja wa Wanafunzi wabunifu wa Chuo hicho Lubna Fatawi kassim ambaye ni Mbunifu wa Mfumo wa Uuzaji wa vifungua kinywa aina ya chai ya rangi,maziwa na kahawa mfumo  unaouza Chai kwa  njia ya sauti amesema Mradi hui unatumia sensa ya sauti pamoja na sensa ya utiaji pesa ambao utaamruhusu mteja kupata huduma anayohitaji.


 Lubna anasema kuwa ubunifu ni sehemu ya maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla jambo ambalo litarahisisha huduma mbalimbali kufanyika kwa haraka na siyo kuweka foleni.


“Nimebuni huu mradi kuokoa foleni mahotelini,maofisini,kwenye sherehe,mashuleni pamoja na sehemu mbalimbali zenye mkusanyiko wa watu kuondoa foleni na watu kupata huduma haraka, lakini huu mfumo ukiomba chai au kahama kwa njia ya sauti unatakiwa kuongea au kuomba huduma kwa mfano Naomba chai,itakujibu karibu tukuhudumie,weka pesa tukuhudumie na ikishaweka tu pesa chai inawekwa kwenye kikombe na mwishoe inakuambia asante umeshapata huduma,"alifafanua Lubna.


 kwa upande wake Mwanafunzi mbunifu Peter Petro aliyebuni mfumo wa kuzima umeme kwa njia ya tovuti ( Website) kwa kutumia simu ya mkono i ni mfumo mzuri ambao utamuwezesha mtu kuzima vifaa vya umeme vya nyumbani akiwa sehemu yoyote jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa jamii.

Naye Mwanafunzi mbunifu Irene kiria  amebuni mfumo wa umwagiliaji wa moja kwa moja kwenye Shamba, Bustani mfumo ambao unatumia sensa ya kupima unyevu kwenye udongo na endapo itabaini udongo ni mkavu sensa itafanya mawasiliano na pampu ili kuruhusu maji kutoka kwa ajili ya kumwagilia shamba au bustani.


Irine anasema mfumo huo wa umwagiliaji ni miongoni mwa mifumo inayorahisisha kilimo kwa kuwa mfumo huo unaruhusu shamba au hustani kujimwagilia wenyewe hata kama muhusika ukiwa mbali.


 Wiki ya kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) imeanza jana tarehe 16 Mei, 2022 na inatarajia kukamilika Mei 20,2022.


Imetolewa na :

Kitengo Cha Habari na Mawasiliano,

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

17.05.2022

Share To:

Post A Comment: