Julieth Ngarabali, ,  Mkuranga. 


Serikali Mkoani Pwani imewaonya baadhi ya waajiri walio chini ya Mkoa huo kuacha mara moja tabia ya kukandamiza wafanyakazi na kusema ifike mahala viongozi walioaminiwa na Rais katika kumsaidia na kuwatumikia wananchi watimize wajibu wao na kama hawawezi basi wapishe .


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema hayo Mkuranga kwenye sherehe za Mei mosi baada ya kupokea malalamiko ya kuwepo kwa baadhi ya waajiri mkoani humo wasiotimiza wajibu wao wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri kutangaza kutoa zawadi kwa watumishi hodari lakini hawakamilishi, mafao na fedha za kuwarudisha makwao wastaafu kuchelewa mara baada ya kustaafu .


 Mei mosi Pwani imefanyika sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Zimamoto na uokoaji yaliyoratibiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo kwa lengo kutoa elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majaga ya moto na kutoa elimu kwa jamii kuhusu majukumu ya Jeshi hilo na namna ya kupata huduma kupitia namba  114


"Siku ingine Wafanyakazi msiniletee risala ya jumla, sema Mkurugenzi fulani, taasisi fulani ,shirika fulani  ,wakala fulani hajatekeleza hiki na hiki na mimi (RC) nitawaambia wajibu malalamiko yenu hapa hapa ,si ndio hivyo ?tufike mahala tulioaminiwa na mheshimiwa Rais kumsaidia,tulioaminiwa kuwatumikia wananchi basi tufanye wajibu wetu"alisema Kunenge


Alibainisha kuwa viongozi wanaotakiwa kukagua mikataba na kuhakikisha watu wana mikataba wapo na hivyo changamoto yakukosekana mikataba inatakiwa wajibu wao na sio yeye (RC )  Mei mosi na kama hawawezi kazi zao basi watupishe maana haiwezekani wafanyakazi wafanye kazi alafu wakati wote wawe wanalalamika.


" alafu mtu anayelalamikiwa ame relax alafu  Mkuu wa Mkoa aje ajibu malalamiko leo Mei mosi kweli?  sifanyi hivyo thats not my stile kila mtu atabeba mzigo wake umeshindwa kaa pembeni na ndio spirit yangu lazima tuubadilishe mkoa wa Pwani nitasimamai haki zenu sitamuone mtu  sitampendelea mtu"ameongeza Kunenge


Awali Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Mkoani humo limesema mshahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ndio kilio chao na kuiomba Serikali kuona umuhimu wa kuongeza maslahi bora hasa mishahara kama ilivyoahidi mwaka 2021 kuwa itaongeza mwaka huu.


Katika risala yao iliyosomwa na katibu wa TALGWU Ester Mang'ana pia Wafanyakazi hao wameomba mchakato wa kikokotoo kipya ukamilishwe mapema na uwe wenye tija kwa wastaafu hasa kutoa mafao yenye tija na kulipa pensheni zinazoendana na wakati uliopo sasa


Wafanyakazi wamesema nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa Umma na binafsi kwa kipindi kirefu sana Serikali haijapandisha mishahara, mfano kima cha chini sekta binafsi iliongezwa mwaka 2013 miama tisa iliyopita .

 

Aidha taarifa hiyo imeeleza  watumishi wa Umma wana miaka zaidi ya sita bila kupandishwa mishahara yao hivyo wanamuomba Rais Samia kutimiza ahadi yake ili wafanyakazi waweze kuendelea na majukumu yao kwa furaha.


Kuhusu changamoto wamesema  wafanyakazi Mkoa wa Pwani wana changamoto nyingi ikiwemo kutokuongezwa mishahara kwa takribani miaka tisa, upandishaji wa vyeo  na nadaraja kwa watumishi ,ulipwaji wa madeni ya watumishi m waajiri kutokutoa   mikataba ya ajira kwa wafanyakazi hasa sekta binafsi hususan viwandani.


Changamoto zingine ni mafao ya wastaafu kuchelewa mara baada ya wafanyakazi kustaafu, fedha /mafao ya kuwarudisha wastaafu makwao,ucheleweshaji wa zawadi za wafanyakazi hodari kwa baadhi ya waajiri pamoja na mabaraza ya wafanyakazi taasisi nyingi hazifatia sheria za uwepo mabaraza hayo.


Naye Marakibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jenifa Shirima ametumia sherehe hizo kuwawaeleza wananchi na wafanyakazi wote kuwa wiki ya zimamoto itafanyika kuanzia Mei Mosi hadi Nane katika maeneo  mbalimbali mkoani humo kwa kutoa elimu  na kauli mbiu yake ni uchumi imara utajengwa kwa kuzingatia kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto..

Share To:

Post A Comment: