Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Uvccm Mkoa wa Ruvuma  chini ya Mwenyekiti wake  Comredi Raymund Mhenga leo tarehe 30/04/2022 imefanya Uzinduzi wa Jengo lao la Kitega Uchumi na Nyumba ya mtendaji wao.


Uzinduzi huo uliofanywa na Mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Uvccm Taifa Comredi Kenan Kihongosi ulihudhuriwa na Vijana,Wanachama na Makada mbalimbali wa CCM ,ambapo Mgeni Rasmi aliwapongeza Uvccm Mkoa wa Ruvuma kwa kutimiza maadhimio ya Baraza kuu la Uvccm Taifa kuhusu ubunifu na uanzishwaji wa Miradi na Ujenzi wa Nyumba za Makatibu wa Jumuiya wa Ngazi za Mikoa na Wilaya kote nchini. 


"Ujenzi huu wa Miradi Kama hii unakwenda kuongeza tija kwenye Jumuiya na kuimarisha utendaji Sababu kwenye Ngazi za Mikoa Sasa Jumuiya itaweza kujitegemea kwa mapato,Lakini pia kwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Mishahara kwa watendaji na kama mtendaji wa Jumuiya anapopangiwa kituo Cha kazi na kukuta tayari Kuna nyumba ya kuishi itampunguzia gharama za Maisha lakini pia kuongeza ufanisi katika kazi zake" haya yalisemwa na Mgeni Rasmi huyo.


Comredi Mhenga Mwenyekiti wa Vijana Wa Mkoa aliwashukuru wadau wote waliochangia na kufanikisha kukamilika kwa mradi huo ambao umegharimu shilingi Million 300.Hasa Mshirika Mkurugenzi wa NFS Mwinuka, Kamati ya Utekelezaji ya Uvccm ya Mwaka 2012-2017 ambao ndio waasisi wa Ujenzi wa mradi huu,Kamati ya Siasa ya Mkoa na wadau wengine wote ambao pia walipatiwa hati ya pongezi.Lakini pia wadau wote waliochangia Ujenzi wa Nyumba ya Mtendaji ambao Umegharimu kiasi Cha shilingi Million 29 na Nguvu shirikishi.


Kamati ya Utekelezaji ya Uvccm Mkoa wa Ruvuma imesema itaendelea kuunga Mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Vijana wa Mkoa wa Ruvuma wanaendelea kukipigania na kukilinda Chama Chao,lakini zaidi kuhakikisha Jumuiya unazidi kuwa Imara kwa Maslahi Mapana ya Vijana wa Mkoa wa Ruvuma.


Imetolewa na Katibu Hamasa na Chipukizi

Uvccm Mkoa wa Ruvuma











Share To:

Post A Comment: