MKURUGENZI wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Rajab Moses Mabamba akizungumza leo wakati wa kongamano hilo Jijini Arusha
Afisa Utumishi wa Manispaa ya Temeke Bihagwa Yogwa akizungumza leo mara baada ya kongamano hilo
MKURUGENZI wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Rajab Moses Mabamba kushoto akiwa kwemye mkutano huo


NA OSCAR ASSENGA,ARUSHA

MKURUGENZI wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Rajab Moses Mabamba amewataka maafisa rasilimali watu (Maafisa Utumishi) nchini kubadilika na kutumia taaluma zao kusaidia kuleta matokeo chanya ya taasisi wanazozisimamia na siyo ukwamishaji

Huku akiwaambia kwamba kazi ya maafisa rasilimali watu ni kusaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa taasisi pamoja na ule wa rasiliamali watu kwa kuwa maafisa hao ni wadau muhimu kwenye usimamizi wa rasilimali watu na uleta tija .

Rai hiyo aliitoa leo kwenye Kongamano la kuazimisha siku ya Kimataifa ya Wataalamu wa  Rasiliamali Watu na Utawala Duniani ambalo huazimishwa kila Mei 20 Duniani ambapo kwa hapa nchini linafanyika kwa siku tatu Jijini Arusha na kushirikisha washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi.

Alisema lazima maafisa rasilimali watu wahakikisha wafanyakazi wanafanya kazi kwa moyo ili kuwasaidia taasisi kuweza kuleta ufanisi na matokeo chanya kwa kuzingatia waledi na ubunifu na hivyo kujenga furaha kwa watumishi wanaowasimamia.

“Kongamano hili ambalo limetuleta pamoja kama maafisa rasilimali watu nchini liwe chachu ya kwenda kuongeza ufanisi na tija katika maeneo yetu mnayotoka lakini kikubwa lazima katika utendaji wenu wa kila siku muwe wabunifu kwa lengo la kujenga uhusiano wa wafanyakazi kufurahia utumishi wao”Alisema Mkurugenzi huyo

Alisema iwapo wakipata ujuzi wa kuweza kuwasimamia wafanyakazi  itawezesha pia kuja na mpango endelevu ambao utawafanya watumishi kuweza kukaa muda mrefu na hivyo kuweza kulitumikia taifa lao kwa tija na ufanisi mkubwa utakaochochea kasi ya maendeleo nchini.

 “Ujumbe wangu kwenu HCR wote tambueni kuwa dunia imebadilika na mnatakiwa kusaidia kuleta matokeo chanya ya taasisi na siyo ukwamishaji wa shughuli za taasisi mnazoongoza”alisema Rajabu.

Awali akizungumza wakati wa kongamano hilo Afisa Utumishi wa Manispaa ya Temeke Bihagwa Yogwa alisema mkutano huo umekuwa sehemu nzuri ya kukutana na itawasaidia kuweza kupata mustakabali kwa namna walivyoweza kuanzisha bodi.

Alisema bodi hiyo itakuwa inaangalia kwa namna watakavyokuwa wakitekeleza majukumu yao kama maafisa  utumishi,rasilimali watu na kufanya hivyo kutaongeza mchango wao utoaji huduma kwenye taasisi za serikali na zisizo za serikali.

Hata hivyo alisema changamoto wanazokutana nazo inatokana na kutokuwa na chambo kimoja ambacho kinasimamia mambo yao kwa hiyo kuwa na vyombo kama miavuli vinakuwa vya shirikisho yanayosimamiwa na watawala  na maafisa rasilimali wao na kuwa na bodi watakuwa na kitu imari na chenye nguvu.

Naye kwa upande wake Katibu Mkuu wa APAT Christopher  Kabalika  aliiiomba Serikali kuona umuhimu wa kuanzisha bodi ya alisema thibati katika kada hiyo ambayo itakuwa mwaroibaini wa changamoto zinazowabili.Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: