Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu, Vijana, Kazi na Ajira, Patrobas Katambi, amesema kwamba zaidi ya bilioni 150 zimekwishatolewa kwa vijana kama mikopo na kusema kama kuna kijana yeyote ambaye hajapata mkopo itakuwa pengine ni Mkenya.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 18, 2022, bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Sophia Mwakagenda, alilohoji kuhusu vijana kutopata ajira kwa zaidi ya miaka 6 sasa pamoja na kwamba mfumo wa utoaji wa mikopo katika Halmashauri kwa vijana mfumo umewatupa nje.

"Sisi kama serikali tunazotakwimu za vijana hawa, na wale wote wanaofanya application za ajira, vyuo vikuu vyote tumekuwa tukipata taarifa, tunao vijana zaidi ya laki mbili wanaoingia kwenye soko la ajira kutoka vyuo mbalimbali, pia tuna mifumo na programu tunazoziandaa ikiwa ni pamoja na internship, kuangaliziwa ajira ndani na nje ya nchi,"amesema Katambia

Aidha Katambi ameongeza kuwa, "Tumekuwa tukiendelea kutoa mikopo na zaidi ya bilioni 150 zimekwishakutolewa kwa vijana mbalimbali, kama kuna vijana ambao wapo labda pengine sio Watanzania ni Wakenya utanisaidia niweze kuwaingiza hapa tuone namna gani tunawasaidia,".

Share To:

Post A Comment: