Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekubali kufanya ushirikiano na Taasisi ya US

PEACE CORPS ya nchini Tanzania inayojihusisha na huduma za kujitolea za Wamarekani katika kuboresha eneo la ujifunzaji na ufundishaji hapa nchini.

Taasisi hiyo ya US PEACE CORPS huleta walimu wa kujitolea nchini kutoka nchini Marekani ambao hufanya kazi za kufundisha katika shule mbalimbali nchini watakazopangiwa walimu hao.

Katika kikao cha mazungumzo kilichomuhusisha Mkurugenzi mwakilishi nchi wa shirika la US PEACE wa shirika hilo Bi.Stephanie Joseph na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba na wadau wengine wa taasisi hizo, wamekubaliana kuwa na ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika kupitia moduli za kufundishia walimu hao wanaojitolea ili ziendane na tamaduni za Kitanzania.

Dkt.Aneth Komba amesema kuwa TET ipo tayari kufanya kazi na taasisi hiyo inayojitolea nchini Tanzania kuimarisha ujifunzaji wa masomo ya Sayansi.

“Tutabadilishana nao uzoefu katika maeneo mbalimbali na hasa eneo la mitaala na kupitia moduli zao za ufundishaji ziweze kuendana na utamaduni wetu”amesema Dkt.Komba.

Walimu wanaokuja kujitolea hapa nchini ni wa masomo ya Sayansi ambayo ni Chemistry, Bilogy,Physics na Mathematics.






Share To:

Post A Comment: