NA HERI SHAABAN (ILALA)


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa vinara wa Usafi kwa kufuata taratibu za usafi ikiwemo kutii agizo la Serikali wasifanye Biashara katika sehemu si rasmi.


Mkuu wa Mkoa Makala aliyasema hayo katika Kampeni endelevu ya usafi Wilaya ya Ilala Kata ya Liwiti eneo la Sigara.


"Kampeni ya pendezesha mji wa Dar es Salaam naomba  iwe endelevu na kuwataka Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Wilaya hii ya Ilala kuheshimu mambo matano  yaliokazawa na Serikali ikiwemo ufanyaji Biashara katika maeneo yaliokatazwa kuweka Biashara kwenye njia ya watembea kwa miguu na katika hifadhi ya Barabara"alisema Makala


Makala alisema Filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuja wakati muafaka ambapo Mazingira ya mkoa Dar es Salaam safi pia yanavutia watalii  aliwapongeza wakazi wa Wakazi wa Mkoa huo akiwemo  MSANII wa KIZAZI kipya Ally Salehe Kiba  kwa kuandaa siku hiyo ya kampeni ya usafi viwanja vya TABATA Sigara .


Mkuu wa Mkoa Amos Makala alisema Jiji la Dar es Salaam limefanikiwa kushika nafasi ya sita katika Bara la Afrika Katika usafi .


Alipiga marufuku Mambo matano* yaliyokatazwa ikiwemo Ufanyaji biashara kwenye *maeneo yaliyokatazwa*, biashara kwenye *njia ya watembea kwa miguu, hifadhi ya Barabara,* Ufanyaji biashara *juu ya Mitaro* pamoja na Ufanyaji biashara *mbele ya Taasisi za umma* ikiwemo Shule.


Aidha  Makalla amepokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya Usafi kutoka kwa Wadau walioguswa na jitihada za Mkoa katika kusafisha mazingira kupitia Kampeni ya safisha Pendezesha Dar es salaam.


Kwa upande wake Msanii Alikiba ameahidi kuendelea kushirikiana na Mkuu wa mkoa Makalla katika kuhakikisha Jiji la Dar es salaam linaendelea kuwa safi ambapo ametoa wito kwa Wananchi kufanya Usafi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kuendeleza usafi katika maeneo yao kila siku Wananchi watakaochafua Mazingira wachukuliwe  hatua Kali.Mwisho

Share To:

Post A Comment: