Na John Walter-Manyara

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Manyara limeanza kuwahudumia wateja wake kupitia mfumo mpya wa kidijitali ujulikanao kama NIKONEKT unaopatikana kupitia App maalum kwenye simu janja na au ya kawaida. 

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo rasmi mei 30,2022, Afisa Uhusiano na Wateja wa (TANESCO) Mkoa wa Manyara Marcia Simfukwe amesema  inamrahisishia mteja  kuokoa muda na gharama kwa kuwa sio lazima afike ofisi za TANESCO.

Amesema kwa sasa mteja popote alipo anaweza kuhudumiwa kwa njia ya mtasndao Kidijitali kupitia App ya NIKONEKT kwenye simu janja au kwa simu zingine kwa kubonyeza *152*00# kisha unachagua namba 4 huku kitambulisho cha NIDA kikitumika katika kujaza taarifa.

"Amesema hii ni NIKONEKT NA BADO,hii ni chap chap,muda wowote mteja anaruhusiwa kuomba akiwa popote" alisisitiza 

Mmoja ya wateja aliyeunganishiwa umeme ndani ya siku moja  Batholomayo Robert mkazi wa kijij cha Singu wilayani Babati amesema alifika TANESCO kupata huduma ambapo alijua angesubiri kupata Umeme baada ya muda mrefu ila badala yake akakuta mambo tofauti.

Mteja huyo ameusifu mfumo huo akieleza kuwa ni hatua kubwa iliyopigwa na shirika hilo kwani awali iliwalazimu kutumia muda mwingi na gharama nyingi za kwenda katika ofisi za TANESCO kujaza fomu hali iliyokuwa ikiwalazimu kusitisha shughuli zingine.

"Nilienda TANESCO leo kujaza fomu nikajua tutakaa muda mrefu kama tulivyozoea kipindi cha nyuma,lakini leo nimekuta mambo mengine mapya,nimejza leo leo,nimefungiwa umeme leo leo,waendelee kuhudumia wananchi namna hii" alisema 

Mfumo wa NIKONEKT App  utakuwa ndio mwarobaini wa kukomesha vishoka kwa sababu mfumo huo ni mteja mwenyewe anaunganishwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco moja kwa moja bila kuwa na mtu wa kati.


Share To:

Post A Comment: