Na Mwandishi Wetu

MWANAFUNZI  wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Sandra Sommi kozi ya Uhandisi wa Komputa leo ameibuka mshindi wa kwanza katika kundi la vyuo vya kati katika mashindano ya Kimataifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2022).


Ushindi wa Sandra unatoka na ubunifu wake wa mashine ya kumsaidia watoto chini ya miaka mitano kupumua (bable CPAP).

Mshindi huyo amekabidhiwa na Makamu wa Rais,  Dkt Philip Mpango hundi ya Sh milioni tano na cheti.

Dkt. Mpango alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo ya Kilele cha Wiki ya Ubunifu Kimataifa yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Jamhuri.Share To:

Adery Masta

Post A Comment: