Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael akiongea na Wajumbe wa kamati ya Taifa ya Maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliyofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Crater jijini Arusha.

Bw. Felix John, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani –Kamisheni ya Afrika amesimama kwa ajili ya kutambulishwa rasmi kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa.


Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mkutano 65 wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Afrika, Bw. Rahim Bhaloo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar akifuatilia maelezo yanayotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Philip Chitaunga akiongea na Wajumbe wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Maandazili ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Afrika

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa, Bw.Felix John (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii (TCT), Bw. Richard Lugimbana, wengine Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Kitaifa, Bw. Rahim Bhaloo (wa pili Kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Philip Chitaunga (wa kwanza kushoto).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Dkt. Francis Michael akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani - Kamisheni ya Afrika.

*****************************

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael amezinduwa rasmi kamati ya Kitaifa ya maandalizi ya mkutano wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika ( 65th UNWTO-CAF MEETING) utakaofanyika Jijini Arusha tarehe 5 – 7 Oktoba, 2022. Mkutano huu wa 65 unakauli mbiu isemayo ‘’Rebuild Africa Tourism Resilian for Africa” unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri wenye dhamana ya sekta ya Utalii na Uhifadhi kutoka katika nchi wanachama wa UNWTO.

“Nategemea kamati hii itafanya kazi kwa weredi, maarifa na kuwa na kasi kubwa katika maandalizi haya. Nipo tayari kushirikiana nanyi muda wowote kwani lazima tuhakikishe kuwa Tanzania inakuwa mfano kwa nchi nyingine wananchama wa umoja huu. Nina nafasi ya kufanya mabadiliko ya wajumbe wakati wowote pale ninapoona maandalizi yanalegalega”, aliyasema hayo Dkt. Francis wakatika wa uzinduzi wa Kamati uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ngorongoro Crater uliopo katika jengo la Kituo cha Utalii Ngorongoro jijini Arusha.

Kamati ya Maandalizi ya Kitaifa ambayo itakuwa na wenyeviti Wenza wawili ambao ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Felix John na mwenyekiti mwenza Bw. Rahim Bhaloo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wataongoza kamati ya wajumbe kutoka kwenye baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliaisili na Utalii, Taasisi na Idara za Wizara mbalimbali, vyama vya wadau wa utalii na waandishi habari wa Tanzania.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Felix John amesema, “Mkutano wa 65 wa UNWTO kufanyika Tanzania ni sehemu ya utekelezaji wa vitendo wa mkakati wa Bodi ya Utalii wa kutangaza na kukuza utalii wa Mikutano (MICE) ambao unalenga kuvutia mikutano mingi ya kimataifa kufanyika nchini Tanzania. Wito wangu kwa wadau wa utalii, wajitayarishe kutoa huduma nzuri kwa ugeni huu ili tuendelee kuiweka nchi ya Tanzania kwenye nafasi nzuri ya kuaminiwa kuandaa mikutano mingine ya kimataifa.

Naye Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT), Rahim Bhallo alieleza kuwa, Mkutano huu ni fursa kwa nchi ya Tanzania kuuza mazao ya utalii na uwekezaji katika sekta ya utalii. Vilevile ni fursa kwa mwananchi wa Tanzania kuwa kuwa wabunifu ili waweze kufanya biashara na kujiongezea kipatao kupitia mkutano huo wa 65 wa UNWTO-CAF.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: