Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nasri Ali (kulia) akimsikiliza Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Stephen Kauzeni aliyeongozana na maafisa wengine (hawapo pichani) kwa ajili ya kuzungumza kuhusu kuanza kwa Kampeni ya Utoaji elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango iliyoanza leo 16 Mei, 2022 wilayani hapo.



Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nasri Ali wakati walipomtembelea ofisini kwake leo 16 Mei, 2022 kwa ajili ya kuzungumza kuhusu kuanza kwa Kampeni ya Utoaji elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango iliyoanza leo 16 Mei, 2022 wilayani hapo.



Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Stephen Kauzeni akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nasri Ali (kulia) mfuko wenye tisheti za "HAKIKI STEMPU" ikiwa ni lengo la uhamasishaji matumizi ya stempu za kodi za kielektroniki (ETS) wakati wa Kampeni ya Utoaji elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango iliyoanza leo 16 Mei, 2022 wilayani hapo.



Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati walipomtembelea ofisini kwake leo 16 Mei, 2022 kwa ajili ya kuzungumza kuhusu kuanza kwa Kampeni ya Utoaji elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango iliyoanza leo 16 Mei, 2022 wilayani hapo.


MKUU wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nasri Ali amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara wanaogeuza maduka yao kuwa Machinga kwa kutoa bidhaa zao kidogokidogo na kuwapa Wamachinga kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.

Kauli hiyo ameitoa leo ofisini kwake Wilayani hapo wakati alipotembelewa na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wapo Wilayani hapo kwa ajili ya Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi iliyoanza leo Wilayani hapo.

Mhe. Khadija amesema kwamba, kumekuwa wimbi kubwa la wafanyabiashara kutoa biashara zao kwa Wamachinga na pia kumekuwepo na uanzishwaji wa biashara ambazo sio rasmi maarufu kama biashara bubu ambazo ndani yake kuna biashara nyingine zinazoendelea ndani yake na hazilipi kodi.

“Kumekua na uanzishwaji wa biashara ambazo sio rasmi, hasasa uwepo wa viwanda ambavyo haviko rasmi na viwanda hivi ndani yake kumekua na biashara nyingine zikiendelea, sambamba na hili kumekua na wimbi la wafanyabiashara wenye tabia ya kutoa biashara zao kwa Machinga wakiwa na lengo la kukwepa kulipa kodi, haya ndo mambo ambayo kwa kipindi kifupi nimeyabaini”, alisema Mhe. Khadija.

Aidha, ametoa wito kwa TRA kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya kodi ya kutosha kwa wafanyabiashara wote ili waweze kulipa kodi zao stahiki na kwa wakati.

Kwa upande wake Afisa Msimamizi Kodi Mkuu wa TRA, Bw. Stephen Kauzeni amesema lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara Wilayani hapo hususani kuhusu urasimishaji wa biashara zao, kusikiliza kero zao na kuzitatua, utoaji wa risiti za EFD pamoja na uhamasishaji wa matumizi ya Stempu za Kodi za Kielektroniki yaani ETS.

“Tupo Wilayani Mkuranga kwa muda wa wiki nzima na tupo kwa ajili ya kuwapatia elimu ya kodi wafanyabiashara wa eneo hili ambapo tunalenga kuhakikisha kwamba wafanyabiashara ambao hawajajisajili wanajisajili kwa kupata Namba za Utambulisho wa Biashara (TIN), wanatoa risiti za EFD, Wanauza bidhaa zenye kulinda afya za mlaji yaani tunahimiza uhakiki wa stempu za kodi za kielektroniki (ETS) pamoja na kusikiliza kero zao mbalimbali na kuzitatua”, alisema Kauzeni.

Nao Wafanyabiashara Wilayani hapo wametoa maoni yao tofauti kuhusu zoezi la kampeni ya Elimu ya Mlango kwa Mlango iliyoanza leo wilayani hapo ambapo wamefurahia elimu hiyo kuwafikia na kueleza umuhimu wake.

Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi ni mwendelezo wa mkakati wa TRA wa kuhakikisha kwamba Wafanyabiashara nchini kote wanapewa elimu ya kodi ya kutosha na hatimaye waweze kufurahia kulipa kodi zao stahiki na kwa wakati ili Serikali iweze kupata mapato na kuleta maendeleo.
Share To:

Post A Comment: