Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa maonesho haya.
Mbunifu Ashirafu Madai Selemani kutoka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kuwezesha magari ya dharura kubadili taa za barabarani {Traffic Light Control for emergency Vehicle"
Mbunifu Nauriya Abbdallah Kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taka.
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo kimeshiriki ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2022 yanayofanyika Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo mgeni rasmi Makamu wa kwanza wa Rais wa  Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amewataka watu mbalimbali wenye uwezo wa kuonesha bunifu mbalimbali kuendelea kujitokeza ili serikali ione namna itakavyowaunga mkono.

Akizungumza akiwa kwenye banda la Chuo hicho Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo kimeendelea kuibua bunifu nyingi zaidi ambazo zitasaidia Serikali katika kuchangia Uchumi wa Kati wa Viwanda.

Prof. Mwakalila amesema Zaidi ya bunifu 20 zinashiriki maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.(MAKISATU).

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.


Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na Mawasiliano

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

16.05.2022

Share To:

Post A Comment: