Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe.Peres Boniface Magiri kukaa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) kuja na njia sahihi ya kudhibiti uzito wa magari badala ya kuweka magoli barabara.

Bashungwa ameyasema hayo jijini hapa wakati wa kuelekeza utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Alisema Serikali imejenga barabara ya lami ya Kidabaga-Bomba la Ng'ombe  kwa kiwango cha lami lakini cha ajabu TARURA wilayani humo imewe magoli barabarani ikiwa ni kimo cha kuzuia ubebaji mzigo mizito.

" Kule Kilolo kuna jambo la ajabu linaendelea, Serikali imejenga barabara ya lami ya Kidabaga hadi Boma la Ng'ombe, jambo la ajabu wameweka magoli barabarani kudhibiti overlord, lakini hawajui kuwa gari linaweza kubebea mzigo mkubwa wa mbao kavu na gari likipita kwenye mizani na likawa na uzito unaotakiwa."

" Lakini pia gari linaweza kubebea mzigo mdogo wa mbao mbichi na uzito wake ukawa ni mkubwa kuliko kiwango kinachotakiwa. Kusema ukweli haya magoli yaliyowekwa yanasumbua hata magari ambayo yanavyuma vya juu lakini hayana mzigo."

Kutokana na hali hiyo, Bashungwa aliagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilolo kukaa na TARURA ili kuja na njia nzuri ya kudhibiti uzito wa magari ikiwamo ya kuwa na mizani inayohamishika.

" Serikali imeboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji na kuleta usumbufu kwa wananchi, sasa badala ya kuweka magoli basi waje na njia nzuri ikiwemo ya kuwa na mizani ya kuhamishika."

Share To:

Post A Comment: