Na John Walter-Babati

Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu katika halmashauri ya mji wa Babati Bw. Faustine Masunga , amefariki dunia. 

Alikuwa na umri wa miaka 51.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea usiku wa kuamkia Mei 16,2022.

Awali alilazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa na baadaye hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo alifariki dunia akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Faustine Masunga alikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati tangu alipoondooka aliyekuwa Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko Agosti 2021.

Msiba upo nyumbani kwake katika mtaa wa Bagara mjini Babati.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Share To:

Post A Comment: