AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa Mwalo wa Sahare Jijini Tanga namna ya kuvaa vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini wakati alipokwenda akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga na Mwalo wa Sahare Jijini Tanga mkoani Tanga  kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira

AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa namna ya kuvaa vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini wakati alipokwenda akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga mkoani Tanga  kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa Mwalo wa Sahare Jijini Tanga vifaa vya kujiokolea wanapokuwa baharini ambavyo ni muhimu kuhakikisha wanakuwa navyo kabla ya kuingia majini kufanya shughuli zao wakati wa utoaji wa  elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akisisitiza jambo kwa wavuvi wa mwalo wa Sahare Jijini Tanga wakati wa utoaji wa  elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akisisitiza jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga
AFISA Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akizungumza  jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga
AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina  Miruko akizungumza wakati wa utoaji wa elimu
 kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akifuatilia kwa umakini maswali kutoka kwa wavuvi,wamiliki wa vyombo
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la TASAC Martha Kalvin akieleza jambo kwa wavuvi kuhusu umuhimu wa usalama wawapo kwenye shughuli zao
Sehemu ya wavuvi,wamiliki wa vyombo na manahodha wakimsikiliza Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira.

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesisitiza umuhimu wa wavuvi kuzingatia usalama ikiwemo kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea wanapokuwa katika shughuli za Uvuvi wawapo majini ili kuwaepusha na vifo,majeruhi na kupoteza mali.

Huku wakisisitiziwa umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini ili viweze kuwasaidia kuepukana na ajali ambazo wanaweza kukumbana nazo.

Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua wakati na akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga na Mwalo wa Sahare Jijini Tanga mkoani Tanga walipokwenda kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira.

Alisema kwamba ni muhimu kwao kuweza kuhakikisha wanazingatia usalama wakati wanapokwenda kufanya shughuli zao kwani hilo litawaepusha na majanga ambayo wanaweza kukutana nayo na kupelekea kupata majeraha au kupoteza maisha na mali.

“Serikali imeona hilo ni jambo la msingi sana na ndio maana tumeona leo tuje hapa Monga Vyeru kuwapa elimu hii ya usalama  na utunzaji wa mazingira hususani mnapokuwa kwenye shughuli zenu hili ni jambo hilo lakini pia kuhakikisha mnakuwa na vifaa vya uokozi”Alisema

“Kwani tunatambua kwamba pia wavuvi wana familia hivyo elimu hii itaweza kuwasaidia kupunguza ajali,kuondoa vifo na kupunguza majeruhi na kuacha familia kuwa tegemezi”Alisema

Afisa Mfawidhi huyo alisema shughuli za usalama sio jambo la mtu mmoja bali ni watu wote hivyo lazima wahakikisha wanazingitia sheria za usalama ikiwemo kuvaa majaketi ya kujiokolea "life jacket" ili yaweze kuwasaidia pindi wanapokumbana na dhoruba baharini waweze kujiokoa.

“Lakini pia kuhakikisha tunakuwa tunazingatia usalama tuwapo majini moto unawaka kutokana na mafuta hauwezi kuuzima na maji ni lazima uhakikisha unatumia mchanga au poda maalumu “Alisema

Hata hivyo alisema ni muhimu na vizuri kwa wenye vyombo vinavyotumika kwa ajili ya shughuli za uvuvi wanakuwa na watu wenye ujuzi na kufanya kazi za majini ikiwemo wajibu wa mmiliki kutii sheria bila shuruti kuhakikisha usalama wake.

Hata hivyo Afisa Mfawidhi huyo aliwataka kuhakikisha kabla hawajaingia majini kuendelea na shughuli zao lazima wawe na cheti kutoka kwenye Shirika hilo ambavyo vinawaruhusu kufanya kazi majini.

“Lakini suala jingine sheria imemuelekeza Afisa Uvuvi asipope leseni ya uvuvi mpaka awe amepata cheti cha Shirika la TASAC cha kuruhusiwa kufanya kazi majini ”Alisema

Mwisho.












Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: