Na Ahmed Mahmoud

Zaidi ya mbegu za ngano tani elfu kumi na saba imetolewa kwa wakulima waliojiunga katika vyama mbalimbali vya ushirika.katika mikoa ya Arusha Manyara na Kilimanjaro

Mbegu ambazo zimezalishwa na Kituo cha utafiti wa mbegu TARI Selian  za mazao mchanganyiko  zinatarajiwa kupandwa msimu huu wa kilimo.

Wakati wa wakulima wa ngano  wakianza kuwekeza katika kilimo cha ngano kwa kufuata mbinu za kilimo cha kisasa, ambazo zimetolewa kwa wakulima kabla ya kuletewa hizo mbegu za ngano.


Makala haya yanaelezea mikakati ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kufadhili Mradi huo wa kuzalisha mbegu za zao la Ngano kupitia Kituo cha TARI- Selian

Ngano ni zao la chakula duniani hapa Tanzania hutegemewa Sana kwa kipato na pia kwa chakula katika miaka ya 1990 uzalishaji wake ulikuwa tani elfu sabini hadi tani elfu 80 kwa wastani wa hekta 46,620.Mahitaji ya wakati huo ilikuwa tani 114,000 ambapo pengo la uhitaji lilizibwa kwa uagizaji kutoka nje, uhitaji kwa Sasa umekuwa mkubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wanaohamia mijini ambako matumizi ya vyakula vitokanavyo na Ngano yameongezeka.

Ni Jambo la kawaida mijini kuwa na matumizi ya Ngano kwa chakula ikiwemo mikate maandazi chapata keki nk.,Jambo linalohitaji uhamasishaji wa kutumia Ngano kama chakula ufanyike.

Ngano huzalishwa  katika mwinuko wa (masl) 1280 -1950 toka usawa wa bahari katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania ambapo maeneo ya Hanang Karatu Monduli juu Naberera West Kilimanjaro na baadhi ya maeneo ya Arusha uzalishaji umekuwa chini 

Serikali imeeleza kuwa zaidi ya nusu ya chakula chote kilichoagizwa nje ya nchi kwa miaka sita iliyopita kilikuwa ni ngano ili kukidhi mahitaji ya ndani ya uzalishaji hasa viwandani.Wakulima wanaolima ngano Tanzania wanapishana na fursa ya mabilioni baada ya Serikali kueleza kuwa kiwango wanachozalisha nchini kimeshindwa kukidhi mahitaji ya ndani ya soko na kusababisha sehemu kubwa ya shehena ya chakula hicho iagizwe kutoka nje ya nchi.  


Hatua hiyo imekuja kwa serikali kubainisha  kati ya mwaka 2014 na 2019 chakula kilichoagizwa nje ya nchi kilikuwa na thamani ya takriban Sh7.74 trilioni ikiwemo asilimia kubwa zao la ngano. 


Katika wastani wa kipindi hicho cha miaka sita iliyopita, Tanzania imekuwa ikiagiza wastani wa chakula chenye thamani ya Sh1.3 trilioni kila mwaka.


Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaeleza kuwa kila mwaka Tanzania inaagiza takriban tani 863,000 za ngano nje ya nchi huku uzalishaji wa ndani ukiwa chini ya tani 100,000.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018, mwaka juzi Tanzania ilizalisha ngano tani 57,000 ikilinganishwa na tani 50,000 za mwaka 2017. 

“Lakini ukigawanya hizo takwimu ni chakula gani tunaingiza kwa wingi katika kipindi cha miaka sita? Ngano ni asilimia 53.3,” inaeleza taarifa ya  mkutano huo uliwakutanisha wadau kuzungumzia mikakati ya kukifanya kilimo cha Tanzania kuwa cha kibiashara.


Kwa mujibu wa Mtafiti wa Mazao ya Shayiri na Ngano wa TARI-Selian Agnes Muniss anasema kwamba mbegu hizo za ngano ya chakula, zina ubora wa hali ya juu kutokana na kuwa na protini ya kutosha, hivyo ngano itakayovunwa, inafaa zaidi kwa  matumizi ya nyumbani na viwandani, ambako hutumika kutengeneza mikate, keki, chapati na vyakula vingine.


kuna tani elfu thelathini na saba zinazotarajiwa kuletwa ili kuendana na mahitaji ya wakulima waliojiunga katika vyama vya ushirika.

Taarifa yake Mtafiti umuhimu kwa wakulima wanapaswa kuzalisha ngano yenye ubora inayoendana na mahitaji ya soko, kufanya hivyo itasaidia kukuza na kuimarisha soko la ndani la ngano.

"Inampasa kama mkulima ataweza kufuata masharti ya kilmo cha kisasa kwa hekari moja kuna uwezekano wa kupata gunia 25. Hayo yakiwa ni makadirio ya kiwango cha juu kwa uzalishaji na kiwango cha chini cha uzalishaji ni gunia 12, "


"Sisi TARI-Selian tumejipanga kuazalisha kwa kushirikiana na makampuni mbegu bora za Ngano kwa Lengo la kupunguza wigo wa ununuzi nje ya nchi wa zao hilo'

Watafiti wa kituo cha selian wakaja na ubunifu wa Mradi wa kuwawezesha wakulima kuzalisha aina bora za mbegu zilizozalishwa na kituo cha Utafiti SARI.


Mradi huo wa uzalishaji mbegu kwa wakulima kufundishwa kanuni za uzalishaji kwenye Mwaka wa 2009 na Mradi huo umeendelea kupanuliwa hasa baada ya kuonyesha muitikio mkubwa wa wakulima wa wilaya ya Karatu.Aidha baada kuvuna wateweza kuuza kwa wakulima wenzao wa Ngano ili kuongeza uzalishaji kwa ujumla ambapo Mradi huo unafadhiliwa na NZARDEF na umenza na wakulima wa wilaya Karatu mkoani Arusha.


Aidha wakulima hao wamefundishwa kanuni za uzalishaji ulionza Mwaka 2009 huku Mradi huo ukiendelea kupanuliwa hasa baada ya kuonyesha muitikio mkubwa wa wakulima wa wilaya ya Karatu.

Uzalishaji wa zao la Ngano maeneo ya Naberera na West Kilimanjaro bado yapo chini ya wakulima wakubwa huko maeneo yaliobakia yakiwa katika vyama vya ushirika.

"Suala hili la wakulima kufundishwa uandaaji wa kuzalisha mbegu ilitokana na magonjwa,kuonyesha uzaifu, pia gharama kubwa ya usafirishaji,kwa mbegu walizokuwa wanajizalishia wenyewe na hivyo kukosa ubora na mavuno mengi".Anaeleza Mtafiti Munissi kutoka taasisi ya Tari Selian

NUKUU; Wizara ya kilimo imeeleza kuridhishwa na uwekezaji wa kilimo cha mazao ya kimkakati ya kitaifa ya shayiri na ngano katika shamba kubwa la Matadi wilayani Siha mkoani kilimanjaro.

Kadhalika serikali imesema iwapo uwekezaji huo utafanywa katika mashamba yote nchini  yaliyokuwa ya serikali na kuingia mkataba na wawekezaji taifa litafikia malengo ya kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka na kujitosheleza kwa ngano ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa kwa nyakati tofauti na mkurugenzi wa maendeleo ya nafaka Bw. Nyasebwa Chimagu baada ya kutembelea na kukagua kilimo cha mazao hayo katika shamba hilo na kujionea ngano na shayiri ilivyostawi.


Bw. Chimagu, ambaye yupo katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa kwenye mkutano wa wadau wa ngano na serikali juu ya uzalishaji wa zao hilo atafanya ziara kama hiyo katika mikoa ya Arusha, Manyara na mikoa ya nyanda za juu kusini yenye mashamba makubwa yanayolima zao hilo.


Mwekezaji mzawa wa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 342, Bw.Henry Mosha ameipongeza serikali kwa kuwawekea mazingira rafiki wawekezaji na wakulima wa mazao hayo kwa kuingia mikataba na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.

Kwa mujibu Mosha Makubaliano hayo, serikali inawapatia mbegu na pembejeo na kuishauri serikali kuwa na  utaratibu huo baada ya kuingia mkataba na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ili uwe wa kudumu.

Huu ndio mkakati wa serikali ya awamu ya sita wa kuhakikisha zao la Ngano na Shayiri  yanakidhi soko la ndani ifikapo Mwaka 2025 kwa kuongeza nguvu kwa wakulima kufikia uzalishaji wa tani milioni 1


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: