Na.WAF-Dar ea Salaam


Serikali kupitia Wizara ya Afya ipo mbioni kuanzia huduma za kliniki tembezi Kwa akina mama wajawazito wanakaribia kujifunga katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi.


Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Italcoser Worldwide Services (ISW) ya nchini Itali Bw. Claudia Fava


Viongozi hao wawili wamekubalina kuanzisha mashirikiano hayo  katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Sita za kuimarisha huduma za afya zilizo na ubora, vilevile kuanzia shirika la IWS  hapa nchini ambalo litajihusisha na huduma za Kliniki tembezi za afya ya uzazi,mama na mtoto ambazo pia zina vyumba vya upasuaji kujifungua na zimeunganishwa na teknolojia ya tiba mtandao.

Share To:

Post A Comment: