Katibu Tawala mkoa wa Arusha Dr.Athman Kihamia (mwenye Shati la Kitenge) Akiwa pamoja na mwenyekiti wa Taasisi ya Tuelekezane Peponi,bw.Nassir Al Jahadhamy pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwl.Zainab Makwinya katika kikao kilichofanyika Ofisini kwa Katibu Tawala.


Na.Ashura Mohamed,Arusha

Taasisi ya dini ya kiislamu inayojulikana Kama Tuelekezane Peponi imetoa msaada wa kuchimba kisima cha Maji katika shule ya sekondari maalumu ya Patandi iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.


Wakizungumza mbele ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha dkt.Athmani Kihamia,Nassir Jahadhamy ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi hiyo alisema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa Taasisi hiyo kusaidia jamii ili kuhakikisha kuwa wanapata maji Safi na Salama.

Bw.Nassir alisema kuwa kisima hicho Cha Maji kitagharimu kiasi cha shilingi Milioni 8 za kitanzania na tayari utekelezaji wa uchimbaji umekwishaanza.

"Hiki ni kisima cha 50 tumekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii na shule hii ni muhimu kwa kuwa ina watoto wenye ulemavu,hivyo tukiwasaidia haya maji wataweza kusoma vizuri tunaamini hivyo na tuendele kushirikiana"alisema Al Jahadhamy

Kwa upande wake katibu Tawala mkoa dkt.Athman Kihamia ameishukuru taasisi ya Tuelekezane Peponi kwa msaada huo ambapo alisema kuwa jumla ya watoto 280 wenye nahitaji maalumu wanapatiwa elimu hapo huku watoto 216 wanalala bweni.

Dkt.Kihamia aliwataka wadau hao kuendelea na moyo huo huo wa kusaidia jamii hata katika maeneo mengine kwa kuwa serikali ina mashirikiano mazuri na wadau wengine wa maendeleo.

Naye Mwalimu Zainabu Juma Makwinya ni mkurugenzi wa halmashauri ya Meru alisema kuwa shule ya sekondari Patandi ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa maji ambapo kisima hicho kitaondoa kabisa changamoto ya maji shuleni hapo.

Aidha alisema kuwa huo ni sadaka tosha kwa kuwa umekuja kwa wakati muafaka baada ya wao Kama wadau kupeleka mahitaji na kukutana na wadau wa Taasisi hiyo shuleni hapo na kukubali Ombi la mkuu wa shule kuchimba kisima hicho.

"Kisima hiki tumepata kufuatia Sisi wadau ambao tulikusanyana na kupeleka mahitaji shuleni pale Kisha tukakutana na wadau hawa ambapo nao walaileta futari kweli tunashukuru Sana Mana mwalimu mkuu alileta Ombi la kuchimbiwa kisima na wadau wamekubali leo wanatuchimbia,Tunashukuru mno".Alieleza mwl.Zainab

Tuelekezane Peponi ni Taasisi yenye makao yake nchini Oman ambapo imejikita kusaidia jamii katika upande wa kuchimba visima na chakula ambapo mpaka Sasa wamekwishafika katika nchi kama Kenya,Somalia,Yemen,Palestina,India na Oman.



Share To:

Post A Comment: