Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza na Watendaji wa Manispaa ya Kinondoni mara baadaya kumaliza Ziara yake leo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukasirishwa na mwenendo usioridhisha wa zoezi la anuani za Makazi Kutokana na Kasi ya zoezi hilo kuwa ndogo.

RC Makalla amesema hayo wakati wa majumuisho ya ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Kinondoni ambapo ameelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa zoezi hilo kwa kulifanya kuwa agenda muhimu na Kila siku watoe taarifa kwa ya mwenendo wa zoezi kwa Katibu tawala wa Mkoa huo.

Aidha RC Makalla amesema Mpaka tathimini ya mwenendo wa zoezi inaonyesha Wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa 33%, Kigamboni 27%, Temeke 20%, Ubungo 11% na Halmashauri ya Jiji la Ilala inaburuza mkia kwa 7% ambapo amekerwa na baadhi ya Halmashauri kusuasua kuwalipa Vijana Wanaofanya zoezi hilo.

Hata hivyo RC Makalla amesema Halmashauri za Dar es salaam Zina nyenzo zote na Mazingira rafiki ya kuweza kufanya Vizuri kwenye zoezi hili hivyo hakuna sababu yoyote ya kusuasua kwa zoezi hilo kwenye Mkoa huo.

Share To:

Post A Comment: