Na,Joel Maduka Geita….


Shirika la Plan International Mkoani Geita  leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari  Mkoani Geita kwa lengo la kujua masuala mbali mbali ya ukatili dhidi ya watoto.


Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo ,Mratibu wa mradi wa Jinsia  na Ujumuishi kutoka kwenye shirika hilo  Zamda Magowa  amesema lengo kubwa la kukutana na wanahabari ni kuona namna gani wanaweza kushiriki na kuibua masuala mbali mbali ya ukatili wa kijinsia ambao umekuwa ukiwakabili watoto wadogo kwenye jamii ambayo wanafanyia shughuli zao.


"Shirika letu limekuwa na malengo makubwa ya kutaka kuwasaidia watoto na kubwa ni kuondokana na ukatili wa kijinsia ambao tumeona ni tatizo kubwa kwenye jamii yetu waandishi ndio watu ambao wamekuwa wakiibua masuala mbali mbali ya Kijamii na tunaamini kupitia mafunzo haya ya siku tatu yatawasaidia waandishi kuibua masuala mbali mbali ya ukatili wa kijinsia na kusaidia kutoa elimu kwa jamii kuondokana na tatizo la ukatili kwa watoto wadogo” Zamda Magowa Mratibu wa Jinsia na ujumuishi wa Plan International Geita.


Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Geita,Frank Moshi ,amesema  bado jamii kubwa imekuwa na upendeleo kwa watoto kwa dhana ya ubaguzi kutokana na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiamini kuwa mtoto wa kiume awezi kufanya majukumu ya mtoto wa kike hali ambayo imeendelea kuwakandamiza watoto wengi wa kike.


“Tunataka kuona sasa jamii inaondokana na mfumo wa ubaguzi wa Kijinsia ikiwezekana watoto wote wapewe haki sawa bila ya kuwepo kwa upendeleo wowote ndani ya jamii yetu” Frank Moshi Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Geita


Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yameanza leo yamewakutanisha waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali kutokana  ndani ya Mkoa wa Geita yakiwa na madhumuni ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuibua masuala mbali mbali ya ukatili wa Kijinsia katika Jamii yetu.

Mwisho

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: