Na,Jusline Marco:Arusha

Waziri wa habari ,mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe.Nape Nauye ameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa zoezi la Anuwani za makazi katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa asilimia 99.1.

Akizungumza jijini Arusha katika muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa zoezi la Anuwani za makazi katika baadhi ya Mikoa ambapo amesema katika mikoa aliyotembelea amebaini uwepo wa changamoto katika baadhi ya taasisi ikiwemo taasisi ya TANROAD na TARURA kuweka majina kwenye barabarani zao.

"Hili ni agizo lililotolewa na Waziri Mkuu kwamba TANROAD  na TARURA kwasababu barabara nyingi niza kwao ili isaidie kasi ya kukamilisha zoezi hili."Alisema Mhe.Nape


Mhe.Nape amesema katika Mkoa wa Tanga utekelezaji wa zoezi hilo haujaenda vizuri hivyo kupelekea kuwa mkoa wa pili kutoka mwisho ambapo baada ya mazungumzo wameahidi hadi kufikia tarehe 18 mwezi huu watakuwa wameongeza hatua.

Aidha ameongsza kuwa ni matunaini yao kuwa maeneo ambayo walikuwa wamekwama watayakwamua na wizara imeahidi kuongeza Nguvu ya utaalamu ili kuwasaidia kuweza kufikia lengo na kukabidhiwa kwa Mhe.Rais mwezi Mei mwaka huu.






Share To:

JUSLINE

Post A Comment: