Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet Kashaigili akifafanua jambo wakati wautoajiwa uwasilishwaji wa matoke ya utafiti wa miaka mitano wa chanzo cha maji cha Jiji la Dodoma Makutupora.

 Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutokaWizaraya Maji Dkt George Lugomela akitoa neno wakati akifungua Warsha hiyo ya siku moja ya kupokea matokeo ya utafiti wa mradi wa GroFutures Jijini Dodoma.

Mtafiti Mkuu wa Mradi huo Profesa. Richard Tayrol kutoka katika Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza akichangia kwenye uwasilishaji wa matokeo hayo.

1Mmoja ya wakulima ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Warsha hiyo kwa niaba ya wa  kulima wengine Dkt. Huruma Msuya akizungumza na SUA MEDIA nje ya Warsha hiyo.

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff cha nchiniUingereza Dkt. Adrian Healy  akizungumza wakati akiwasilisha sehemu ya utafiti wake.

Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi, Watafiti pamoja na wadau wengine kutoka sekta mbalimbali walioshiriki katika warsha hiyo ya kutoa matokeo ya utafiti huo.

1.     Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.


Amina Hezron na Calvin Gwabara, Dodoma.


MATOKEO ya Utafiti yanaonyesha kuwa shughuri za kibinadamu zinazofanyika katika maeneo ya dakio bonde la maji chini ya ardhi la makutupola ambalo ndio chanzo kikuu cha maji cha Jiji la Dodoma zinauwezekano mkubwa wa kuathiri uwepo wa chanzo hicho cha maji endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kulinda chanzo hicho.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mtafiti kutoka katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet Kashaigili katika warsha ya mawasilisho ya matokeo ya Utafiti ulioangalia maji chini ya ardhi katika ukanda wa kusini mwa la Sahara mbele ya wadau wa chanzo hicho cha maji uliofanywa na Watafiti wa SUA kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cardiff na Chuo Kikuu cha Jiji la London Uingereza.

Prof.Kashagili amesema kuwa bila kukaa kwa pamoja kujadiliana namna bora za kulinda eneo hilo sasa chini ya mpango wa upangaji wa Makazi, athari yake itakuwa kubwa ambayo itapelekea kulipa pesa nyingi huko baadae.

“Kuna haja ya kuyaangalia haya mapema ikiwezekana bonde hili litangazwe lote kwenye Gazeti la Serikali kuwa sehemu ya hifadhi ya bonde na liangaliwe kwa upekee wake ili kuzuia shughuri za kibinadamu ambazo zinaweza zikaathiri eneo lile kutokana na umuhimu wake kwakuwa kimsingi ukiangalia tathimini ya maji  mbalimbali  ambayo yametokana na vyanzo mbalimbali karibuni zaidi ya  asilimia 90 za maji ya mji huu wa Doodoma yanatoka pale ”, ameeleza Profesa Kashaigili.

Aidha Prof Kashaigili ameongeza kuwa kwakuwa mvua kwa miaka ya karibuni hazijawa kuwa kufikia zile za El nino zinaweza tumiaka mbinu zingine ambazo zimetumiwa nan chi zingine duniani za kuchimba visima na kuruhusu maji kujaa kwenye eneo hilo na kuyaacha yaingie kwenye mwamba huo ardhini na kisha kuweza kuyatumia kupelekwa kwenye maeneo mengi zaidi ya jiji la Dodoma.

 “Inawezekana haya maji tukayatathimini ubora wake lakini tukayaruhusu yakakaa juu ya ardhi  kwakuweka mazuio mbalimbali ili yaweze kunywea kuingia ardhini jambo ambalo nchi mbalimbali zimefanya hivyo na zimefanikiwa kuondoka na adha zilizopo za upatikanaji wa maji”, alifafanua Profesa  Kashaigili. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji Dkt George Lugomela ameeleza kuwa kwa siku jijini Dodoma linahitajika mita za ujazo 133,845 upatikananji wake ni mita za ujazo 66,600 kwa siku ambayo ni kama nusu ya mahitaji na hii ni kutoka na ongezeko la watu katika jiji hilo.

“Serikali tayari imeweka mikakati Madhubuti katika kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa ikiwemo kuchujenga bwawa la FAKWA lakini mkakati wa haraka ni kuchukua maji mita za ujazo 100,000 kwa siku kutoka bwawa la Mtera ambazo ukichanganya na zile 66,600 za sasa unapata mita za ujazo 166,600 ambazo zitakuwa na uwezo wa kukidhi kabisa mahitaji ya Jiji lote la Dodoma” alifafanua Dkt. Lugomela.

Hivyo amesema kuwa matokeo ya Utafiti huo ni muhimu sana na yatatumiwa na Wizara katika kuwezesha kutazama namna ambavyo itawezekana kutatua changamoto hiyo ya maji kupitia chanzo cha Makutupola tofauti na ilivyo hivi sasa.

Nae Mtafiti Mkuu wa mradi huo  Profesa. Richard Tayrol kutoka katika Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Ethiopia pamoja na malengo mengine lakini pia unalenga kuangalia namna maji yaliyo chini ya ardhi yanavyoweza kuchangia katika kuondoa umasikini.

Ameeleza kuwa maji ya chini ya ardhi hayawekewi mkazo sana kama ilivyo kwa maji ya juu ya ardhi hivyo ameishauri Serikali kuwekeza katika maji yanayopatikana chini ya ardhi kakuwa kuna maji mengi kuliko haya tunayoyaona juu ya ardhi yanayopita kwenye mito na maziwa.

“Naishauri Serikali kuwekeza nguvu, muda pamoja na kuwajengea uwezo watu wake katika kutambua rasilimali hii ya maji yaliyopo chini ya ardhi maana katika fani ya hydrolojia, kwani itasaidia katika kukabiliana hata na mabadiliko ya tabia nchi na kuchangia katika matumizi mbalimbali kama vile Kilimo,Viwanda na matumizi ya nyumbani ”, alisema Profesa. Tayrol. 

Naye mmoja ya wakulima ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Warsha hiyo kwa niaba ya wakulima wengine Dkt. Huruma Msuya ameishauri Serikali kutenga maeneo maalumu kwaajili ya misitu kilimo cha mbogamboga na matunda kwaajili ya kulisha miji  jambo litakalosaidia mji kuwa na sehemu ya kupumulia. 

“Tusifanye makosa kama yaliyofanyika kwenye Jiji la  Dar Es Salaam ambapo mji umekuwa tu kutoka Kariakoo mpaka Kibaha  bila kuwa na maeneo yenye mashamba na Misitu, mji usikue tu kuwe na miji midogo midogo pembeni ya mji mkubwa ambayo nayo itakuwa imeendelea itakuwa inapata maji hukohuku kupunguza hali ya upatikanaji wa maji kutoka upande mmoja”, alisema Dkt Msuya. 

Matokeo ya tafiti yaliyowasilishwa  ni matokeo ya Uafiti iliyofanyika kwa miaka mitano na mradi wa GroFutures ulioanzishwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Chuo cha Cardiff kilichopo nchini Uingereza pamoja na  Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza .


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: