Taasisi isiyo ya kiserikali ya Maryprisca Women Emporment Foundation(MWEF) imekabidhi msaada wa fedha za matibabu kwa Frenzia Ngela mkazi wa Pambogo Kata ya Iyela Jijini Mbeya ambaye mwanawe anasumbuliwa na maradhi ya tumbo.


Akikabidhi msaada huo nyumbani kwa mama huyo Katibu wa Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Maryprisca Mahundi ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, Miriam William amesema taasisi ilipokea maombi kutoka kwa mama huyo baada ya kukosa pesa za matibabu.


Aidha amesema lengo la taasisi ni kuwafikia wanawake wote wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa.


"Taasisi imekuwa ikisaidia watu mbalimbali wenye uhitaji baada ya kujiridhisha na uhitaji huo"alisema Miriam.


Akipokea msaada huo mama wa mtoto huyo Frenzia Ngela ameishukuru taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation kwa kutoa msaada huo mara baada ya kupeleka maombi.


"Kipekee namshukuru Mheshimiwa Maryprisca Mahundi kupitia taasisi yake kwa kuitikia haraka ombi lake"alisema Ngela.


Aidha amesema amepeleka maombi kwenye taasisi nyingi lakini hajapata majibu lakini kupitia msaada uliotolewa na taasisi ya MWEF utasaidia kuokoa maisha ya mwanae.






Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation hivi karibuni ilitoa msaada kwa mwanamke mwingine aliyekwama pesa za matibabu ya upasuaji wa tumbo ambapo hivi sasa afya yake imeimarika baada ya kupata matibabu.


Share To:

Post A Comment: