Raisa Said,Tanga


Jiji la Tanga limejipanga kupunguza suala la udumavu kutoka asilimia 34 hadi kufikia asilimia 20 Kwa mwaka huu 2022.

Hayo yamesemwa na Afisa Lishe Jiji la Tanga Mkoani hapa Sakina Mustafa wakati akizungumza na Mwandishi wa habari za watoto kuhusu namna walivyojipanga kupunguza udumavu Kwa watoto waliochini ya umri wa miak mitano

Afisa lishe huyo amesema katika kufikia asilimia 20 hiyo wameanza kutoa elimu katika maeneo tofauti ya Jiji hilo lakini pia zile afua tulizotekeleza zitasaidia kufikia lengo.

Alisema kuwa licha ya udumavu huwezi kuupima Kwa macho kwani unavitu vingi na anaangaliwa mtoto tangu mimba inatungwa,mama anakula nini na baada ya kujifungua mtoto anakula nini kwani zinahesabiwa zile siku 1000 yani tangu mimba inatungwa akiwa tumboni kisha ananyonyeshwa Kwa miaka miwili.

"Katika hizo siku 1000 wanaangalia mtoto anakula nini ,mtoto amenyonyeshwa ule unyonyeshaji wa lazima,je mtoto amepewa vyakula vile vya ziada vile vyamchanganyiko,je mtoto amepata lishe Sasa hii"Amesema Afisa lishe huyo kutoka Jiji la Tanga.

Alieleza kuwa inatarajiwa kufanyika tafiti itakayoonyesha kuwa udumavu unapungia kutoka asilimia 34 au unazidi "Mimi naimani Kwa elimu tuliyotoa na afua tulizotekeleza utakuwa umepungua kufikia asilimia 20 " amesisitiza.

Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyokuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini hapa aliwataka Watanzania wawekeze kwenye sekta ya uchakataji na usindikaji wa vyakula vyenye virutubishi ( lishe) ili kupunguza kiwango cha watu wenye utapia mlo.

Kauli hiyo alitoa kufuatia baadhi ya mikoa nchini ambayo inazarisha chakula kwa wingi kuwa na ongezeko la watoto wenye lishe duni ikiwamo mikoa ya Njombe, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Songwe na kigoma huku mkoa wa Tanga ukiwa ni mkoa ambao awali ulikuwa chini kwa 23% kwa mwaka 2014 lakini kwa miaka ya hivi karibuni mkoa huo umekuwa na takwimu zinazoongezeka hadi 34%.

Mkutano huo ulikwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Masuala ya Lishe wa miaka mitano awamu ya Pili (NMNAP) ,Waziri Mkuu aliitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta ya chakula na lishe kuwekeza kwenye utafiti na uzalishaji wa bidhaa za vyakula vyenye virutubishi.

''Sisi kama Serikali tupo tayari kuwawezesha wawekezaji kuanzia viwanda vidogo hadi vikubwa lakini pia kwa sasa hivi wapo wazarishaji wa mtu mmoja mmoja hususani wanaotengeneza unga na chumvi majumbani , wote hao ni watu muhimu kwetu" alisema Kasimu Majaliwa.

Serikali kupitia program jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto( PJT - MMMAM) 2021/22- 2025/26 inaeleza Kwa maboresho yalioonekana kwenye taratibu za lishe Kwa watoto wachanga na wengine wadogo ni pamoja na unyonyeshaji na lishe ya vyakula vya ziada kuwa na sababu muhimu zilizochangwa katika kupunguza kiwango Cha udavu kitaifa kutoka kutoka asilimia 33.7 mnamo mwaka 2015-16 (TDHS -MIS) hadi asilimia 31.8 mwaka 2018( TNNS ).

Licha ya maboresho hayo ni muhimu kutambua kuwa udumavu mkali Bado unaathiri mtoto mmoja kati ya watoto Kumi asilimia (10.0) nchini kote ,hii inamaanisha kwenye Kila watoto Kumi was umri chini ya miaka 5.1 anaripotiwa kuwa na udumavu mkali.Hii inaashiria kwamba watoto milion tatu walio chini ya miaka mitano chini Tanzania wamedumaa.

Athari ya udumavu inahusishwa na watoto kutokufikia hatua kamilifiu za ukuaji na Hali hii huongezeka kulingana na umri hadi kufikia asilimia 40 au zaidi Kwa watoto wenye umri wa miezi 18.47 Mtoto mmoja kati ya sita mwenye umri wa miezi 24.35 wana udumavu mkali.mikoa iliyoathirika Kwa udumavu zaidi ya asilimia 40ni Njombe asilimia 53.6 ,Rukwa asilimia 47.9,Iringa 47.1,Songwe 43.3, kigoma asilimia 42.3,Ruvuma 41.0,

Hata hivyo Nchini Tanzania kiwango utapiamlo sugu Bado kipo Juu na suala linalotia mashaka ikizingatiwa kuwa udumavu ni Viashiria mojawapo kinasababisha watoto kutofikia hatua timilifu za ukuaji.
Share To:

Post A Comment: