Moses Mashalla,Arusha 


Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati (Ta bora),Isaack Kisiri  amepongeza usharika wa Olosiva mkoani Arusha kwa kusimamia ujenzi wa kanisa la kisasa na kusema kwamba hatua hiyo ni alama nzuri kwa kanisa la KKKT hapa nchini.


Askofu Kisiri alitoa pongezi hizo leo wakati wa ibada ya jumatatu ya Pasaka ambapo alidai kwamba kanisa hilo ni miongoni mwa mitaa ambayo hapo awali ilikumbwa na migogoro ya mara kwa mara hususani katika hatua za ujenzi.


Askofu Kisiri alisema kwamba Ujenzi wa kisasa wa kanisa hilo pindi ukikamilika utakuwa ni miongoni mwa makanisa ya kisasa katika karne ya sasa.



"Ujenzi wa kanisa hili pindi ukikamilika hili litakuwa ni miongoni mwa makanisa bora na kisasa sisi kama walutheri tunajivunia jengo hili la kisasa nawapongeza"alisema Askofu Kisiri


Alisema kwamba hapo awali kanisa hilo lilikumbwa na mgogoro uliosabishwa na mkandarasi aliyetengeneza ramani ya msingi wa jengo ambayo haikuwa sahihi.


Alisema kuwa mkandarasi huyo pamoja na kutengeneza ramani hiyo lakini alidai jumla ya kiasi cha sh,90 milioni na ndipo alipoitisha kikao kuhoji sakata hilo lakini akiwa katikati ya kikao alipokea ujumbe wa uteuzi wa kuwa mkuu wa Dayosisi ya Magharibi Kati (Tabora).


"Mkandarasi alidai milioni 90 nikaitisha kikao kuhoji lakini wakati nikiwa kikaoni nikapokea ujumbe wa uteuzi wa kuwa mkuu wa Dayosisi semeni Ameen"alisema Askofu Kisiri 


Katika somo la jumatatu ya Pasaka Askofu Kisiri aliwataka waumini kuachana na tabia ya ujeuri na majivuno huku akiwataka watambue ya kuwa mali ni vitu ambavyo hupita tu na wajali utu.


Mwisho.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: