Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul.  mgeni rasmi anayetarajiwa kuwa kwenye Kongamano la Fursa na Uhamasishaji wa Utamaduni wa Mtanzania litakalofanyika Machi 26, 2022 Karatu mkoani Arusha.. 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania(TAMUFO) Stella Joel.
Mdau wa Maendeleo hapa nchini Dk.John Lucian atakuwepo kwenye kongamano hilo.
Mwanamuziki Stara Thomas atakuwepo kutoa burudani.

Mlezi wa TAMUFO Dk. Frank Richard.
 Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Ziwa Manyara, Dk.Noella Myonga naye atakuwepo.

Mwanamuziki Hafsa Kazinja atakuwepo kutoa burudani.T

 


Na Dotto Mwaibale, Arusha.

 

UMOJA WA WANAMUZIKI Tanzania (TAMUFO) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wanatarajia kufanya kongamano kubwa la fursa. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema kongamalo hilo linalojulikana kama Kongamano la Fursa na Uhamasishaji wa Utamaduni wa Mtanzania. 

Alisema kongamano hilo litakalofanyika Machi 26, 2022 wilayani Karatu mkoani Arusha litaenda sambamba na kutembelea Mbuga ya Wanyama ya Ziwa Manyara. 

Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul. 

Aliwataja wanamuziki watakaotoa burudani kuwa ni Mwanamuziki nguli wa kizazi kipya Stara Thomas kutoka Dar es Salaam ambaye ataongoza msafara wa kwenda kufanya utalii wa ndani Ziwa Manyara. 

Alimtaja mwanamuziki mwingine kuwa ni Hafsa Kazinja ambaye amejiandaa vizuri kutoa burudani safi siku hiyo ya kongamano hilo. 

Alisema wahusika wote watakutana Karatu ambako kutakuwa na mambo lukuki huku zikipatikana fursa mbalimbali kama za Bima ya Afya ya NHIF sanjari na kupatiwa elimu kutoka kwa wadau wa maendeleo ambazo zitatolewa kwa wanamuziki na wanajamii kwa ujumla. 

Joel alisema Baraza la Sanaa Tanzania  ( BASATA) na Chama cha Hatimiliki Tanzania  (COSOTA)  watakuwepo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu utolewaji wa mirahaba na usajili wa wasanii. 

Alisema Watu wa Makumbusho ya Taifa pia watakuwepo na watatoa elimu ya uhifadhi wa Utamaduni wa Mtanzania na Uanzishwaji wa Makumbusho mbalimbali zikiwamo za Wanamuziki. 

" Kongamano la namna hii halijawahi kutokea ni la mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi yetu" alisema Joel ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wakiwepo wanamuziki na kwa mawasiliano zaidi ya kujua kongamano hilo unaweza kupiga Simu namba 0756846166 au 0712781171.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: