NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete ameyataka mabaraza yote ya ardhi kuhakikisha yanajikita zaidi kutoa usuluhishi na maamuzi sahihi kwa kuzingatia sheria lengo ikiwa ni  kupunguza migogoro.



Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata ya miono yenye lengo la kuweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafuti ufumbuzi.


 Ridhiwani katika ziara hiyo ameweza kuzungumza na wananchi mbali mbali wakiwemo wazee mashuhuri kutoka  Vijiji vya Kwaikonje, Masimbani pamoja na miono na kusikiliza kero zao.



"Niyaelekeze Mabaraza ya ardhi msiende mkafanya kazi ya kuamua juu ya nani ana haki  a nani hana katika ngazi ya Kijiji na Kata jukumu lenu ni kupatanisha kumua kwa busara "  alisema

Naibu Waziri huyo alisema Mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata kwa mujibu wa sheria  ni mabaraza ya usuluhishi na upatanishi na kwamba wenyeviti wa Mabaraza hayo wanatakiwa kujikita katika nafasi zao za kuwa wenyeviti wa vikao vya usuluhishi na si kutoa maamuzi.

"Nimekutana na lundo la malalamiko ndani ya ofisi yangu, mabaraza yetu ya ardhi mara nyingi hayaonekani kutenda haki katika maeneo yetu na watu wengi wanayalalamikia  hilo ni kwa upande mmoja upande wa pili wasimamizi wa sheria hatutoi tafsiri ya sheria yanatakiwa kufanya nini" alisema.



"Mabaraza ya maamuzi ni kwa ngazi ya kuanzia wilaya kwenda juu tunahitaji kufanya kazi kubwa kumaliza migogori ya ardhi" alisisitiza Ridhiwani.

Alisema kunahitajika kufanya semina na kupeana elimu ya mabadiliko ya sheria na namna mabaraza yanavyotakiwa kufanya kazi ili kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea.


Akizungumzia kuhusiana na kero nyingine za wananchi Ridhiwani alisema atahakikisha Taasisi za Serikali zinapatiwa huduma ya umeme, lakini pia utatuzi wa vikwazo katika kituo cha afya Miono vinafanyika kwa haraka.

Diwani  wa Miono Juma Mpwimbwi alimuomba Ridhiwani kutafuta namna ya kumaliza migogoro hiyo kwani wapo wananchi wamevuka mipaka na kuvamia hifadhi ya kijiji na hivyo kusambabisha migogoro kuendelea.

Mpwimbwi pia alimuomba Waziri huyo kusaidia upatikanaji wa watumishi katika kituo cha afya cha Miono kwani waliopo hawatoshelezi mahitaji ya wananch na pia upatikanaji wa jengo la upasuaji kituo hicho.

"Mheshimiwa Mbunge Mama Salma Kikwete alitoa vifaa vya upasuaji miaka minne iliyopita lakini hadi sasa hakuna jengo la upasuaji na hivyo hofu iliyopo sasa ni vifaa hivyo kwenda kuharibika kutokana na kukaa muda mrefu bila kutumika" alisema.

Nao baadhi ya wakazi wa Kata yaMiono walisema  ni vema timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi ikafuatilia suala la migogoro ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.


Share To:

Adery Masta

Post A Comment: