NA. Abel Paul wa Jeshi la  Polisi Mkoa wa Arusha 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO amesema tarehe Tarehe 01.03.2022 muda wa 06:30 mchana huko maeneo ya Ngaramtoni wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata ELIA MBWAMBO (45) mkazi wa Ngaramtoni akiwa anasafirisha madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni mirungi yenye uzito wa 187kg.

Kamanda Masejo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasafirisha madawa hayo maeneo ya Ngaramtoni kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.793 CUY  aina Varian.

Amesema kuwa Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya usafirishaji wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali jijini Arusha.ACP MASEJO 

Ameendelea kusema kuwa   mara baada  ya   pelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya kulitolea maamuzi kisheria.

ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili kutokomeza kabisa uhalifu ndani ya mkoa wetu. Pia niwatake baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya kuacha mara moja tabia hiyo kwani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: