Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameongoza zoezi la Uzinduzi wa Mradi wa Dar es Salaam Water Security uliofanyika leo katika ukumbi wa Hyatt Regency the kilimanjaro uliopo Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na Viongozi kutoka Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo Tanzania Forest Services Agency(TFC), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC), na Mamlaka ya Maji  safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)


Katika Uzinduzi wa Mradi huo uliofadhiriwa na Tanzania Breweries Limeted (TBS) na kutekelezwa kwa Ushiriki wa World Wide Fund, Naibu Waziri Ametoa Pongezi kwa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa juhudi wanazofanya katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinakuwa safi na salama lakini pia amewataka wadau kujitokeza katika zoezi la kupanda Miti Takriban Heka 200.

Share To:

Post A Comment: