************************

Na John Mapepele

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamishna wa Sensa nchini Mhe. Anna Samamba Makinda amekuwa miongoni mwa wageni walioshiriki usiku wa chakula cha pamoja uliowakutanisha wasanii zaidi ya 200 wanaotarajia kutumbuiza kwenye Tamasha kubwa dunia la Muziki la Serengeti linalofanyika jijini Dodoma Machi 12 na 13, 2022.

Dhifa hiyo ya chakula cha jioni imekuwa ya aina yake ambapo wasanii wamepata fursa ya kuelimisha umuhimu wa sensa.

Aidha, kuelekea kesho kwenye tamasha la Serengeti wasanii mbalimbali wakiongozwa na Bushoke wamekonga nyoyo za wa wageni mbalimbali walioshiriki usiku huu.

Mbali na viongozi Wakuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,wageni wengine ni wabunge na wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha na binafsi na watu mashughuli.

Aidha, wasanii wamepata nafasi ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa makampuni walioshiriki.

Baadhi ya wadhamini wakubwa wa shughuli hiyo ni CRDB, NBC na Tigo, DCB, Dstv na NSSF.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: