Na,Jusline Marco:Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema serikali ya Mkoa chini ya Chama cha Mapinduzi imedhamiria kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ili kukamilisha sehemu ya miradi iliyobaki na kuhakikisha kunakuwepo na mabadiliko ya kimaendeleo katika Mkoa wa Arusha.

Mongela ameyasema hayo katika Kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchanguzi kuanzi mwezi Julai 2021 hadi mwezi Februari 2022 ambapo amesema kutoka mwaka 2020 hadi fenruari 2022 sekta ya Elimu imepokea jumla ya fedha shilingi bilioni 46.3  za mpango wa elimu bila malipo kati ya hizo shilingi Bilioni 14.6 kwa elimu za Msingi na bilioni 31.7 elimu sekondari.

Aidha amesema katika kipindi cha miezi 6 cha utekelezaji wa Ilani jumla ya shule mpya 14 zimeongezeka kutoka shule 823 mwaka 2021 hadi kufikia shule 837 mwezi Februari 2022 ikiwa ni shule za msingi huku upande wa shule za sekondari kukiongezeka kwa shule mpya 17 kutoka shule 252 hadi kufikia shule 269 februari 2022.

Ameongeza kuwa uandikishwaji wa watoto katika shule za awali umeongezeka kutoka watoto 56630 mwaka 2021 hadi kufikia 57411 mwaka 2022 ambapo kwa mwaka 2021 idadi ya uandikishwaji kwa wanafunzi wa darasa la 1 imeongezeka kutoka 56602 hadi kufikia wanafunzi 62462 mwaka 2022 kukiwa na ongezeko la wanafunzi 5860 sawa na asilimia 9.4 

Ameongeza kuwa kupitia halmashauri Mkoa umeendelea kutenga mapato ya ndani jumla ya shilingi milioni 884.15 kwa kipndi cha julai hadi februari 2022 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu 158 katika shule za msingi na shilingi bilioni 1.92 fedha za UVIKO kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 96 ya shule shikizi ili kuondoa adha ya mtoto wanaosoma kutembea umbali mrefu kwa kila halmashauri.

Pamoja na hayo amssema shilingi milioni 160 kutoka katika hela za UVIKO zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 2 katika shule 2 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum na shilingi milioni 735.1 ikiwa ni fedha za miradi la lens,mfuko wa elimu,mfuko wa jimbo kwa ujenzi wa miundombinu 70 katika shule za msingi.

Ameongeza kuwa Mkoa umepokea jumla ya shilingi bilooni 162 za ruzuku ya Tozo kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa 13 katika shule za sekondari zilizojengwa kwa nguvu za wananchi,vilevile wamepokea jumla ya sholingi bilioni 4.7 kwa ujenzi wa sekondari mpya 10 kupitia program ya saving ujenzi wa miundombinu ya shule ambapo pia wamepokea milioni 860.5 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika sekondari.

Katika sekta ya Afya,Mongela amesema kuwa kumeongezeka vituo vya kutoa huduma za afya 25 huku hali ya upatikanaji wa dawa ukiongezeka kutoka asilimia 1.2 hadi asilima 25 huku bilioni 3.8 zilitengwa kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya na fedha za tozo shilingi bilioni 1.75 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 7 katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha sawasawa na shilingi milioni 250 kwa kila halmashauri.

Kwa upande wa sekta ya Maji Mijini na Vijijini jumla ya vijiji 304 kati ya vijiji 390 vinahuduma ya maji rasmi na asilimia 69.8 za ya wakazi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi hadi kufikia februari 2022 ikilinganishwa na asilimia 69.2 ya mwaka 2020 ambapo hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Arusha kutoka asilimia 53 hadi kufikia asilimia 69.9 februari 2022.

Sambamba na hayo katika sekta ya uchumi na uzalishaji mali halmashauri ya jiji la Arusha imejipanga kuongea kiasi cha shilingi milioni 500 ilk kuimarisha sekta hiyo ya wafanhabiashara ndogondogo ambapo kupitia sekta hiyo jumla ya viwanda vidogo 120 vineweza kuanzishwa ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji jumla ya hekari elfu 84.33 na jumla ya hekari 21.42 zimetengwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo 16185 Mkoa mzima wa Arusha.

Katika hatua nyingine Mongella amesema sekta ya Umeme vijiji 118 bimefikiwa na huduma ya umeme sawa na asilimia 71 ya vijiji vyote 547 na kusema kuwa sekta ya umeme bado ina changamoto kubwa ambapo amwwakmba wajumbe wa Jalmashauri kuu kusimamia kandarasi hizo ambazo zimeonekana kusuasua kwani malengo ya serikali ni kufikia mwaka 2025 Kinakuwa na umeme wa uhakika.

Awali Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Athuman Kihamia amewakumbusha watendaji walioteuliwa na serikali kuwa waadilofu,wawajibikaji na ambao watazifanya rasilimali kuonyesha matokeo chanya huku wakiyafanya madaraka ya umma kuwa msingi wa maamuzi sambamba na kuwa wafuatiliaji na watathimini katika utekelezaji wa mipango wanayoipanga.

Dkt.Kihamia amewataka watendaji hao kuwa sehemu ya kuthibiti migogoro ya migongano ya kimaslahi ,kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo ipotevu wa fedha za umma sambamba na kuwepo mifumo ya kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi kwa wakati kwa haki na uadilifu.Share To:

JUSLINE

Post A Comment: