Na Ahmed Mahmoud Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala),limeshindwa kuendelea na vikao vyake kwa madai ya kukosekana uwakilishi wa mawaziri wa Nchi sita za jumuia hiyo kwa kutohudhuria vikao Kwa Muda mrefu na hivyo kukosa majibu ya rasimu zinazowasilishwa. Wakiongea katika kikao cha bunge la nne linaloendelea makao makuu ya jumuiya hiyo Jijini Arusha,wabunge hao walidai hawezi kuendelea na kikao hicho cha bunge kwa kuwa rasimu zilizokuwa ziwakilishwe bungeni zimekosa uwakilishi wa mawaziri au wawakilishi wao . Mbunge wa bunge hilo, Kenneth Kilonzo Muthioka kutoka nchini Kenya amesema hatua ya mawaziri kukosekana katika vikao vya bunge kunasababisha malengo ya bunge hilo kutotimia Kwa wakati. Akitolea mfano ripoti iliyokuwa iwasilishwe bungeni hapo Jana kuhusu gharama za usafiri wa ndege kwa wananchi wa nchi za EAC ni kubwa na zinahitaji majibu ya mawaziri ili wananchi waweze kusafiri Kwa gharama nafuu. “Kwa mfano gharama za kutoka Nairobi kwenda Arusha Kwa ndege ni ghali zaidi kuliko kutoka Nairobi kwenda Dubai”amesema. Naye Mbunge wa Eala nchini Tanzania,Mariam Ussi Yahaya,amesema kuwa kikao Cha bunge waliokuwa wajadili ripoti nne zikiwemo mbili zilizokuwa ziwasilishwe na mawaziri wenyewe na moja ni ripoti ya kamati ya mahesabu ,ambazo zote zimekwama Kwa sababu ya mawaziri kutohudhuria vikao. Amesema kuwa, moja ya ripoti zilizokuwa zijadiliwe ni pamoja na suala la sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinapaswa zianze pia kutumika kwenye nchi wanachama. “Hoja nyingine zilizokuwa zijadiliwe ni mswada wa usafiri wa anga Kwa kutumia ndege (cassoa)ambao imeonekana kuwa ni usafiri ghali zaidi Kwa nchi za Jumuiya hiyo ,na hivyo kuwaumiza wananchi wetu ambao wamekuwa wakisafiri kufanya biashara na wanafunzi kwenda kusoma kwenye nchi wanachama”amesema. Amesema ripoti inaonyesha kuwa usafiri ndani ya Nchi wanachama wa EAC ni ghali Sana suala ambalo lilipaswa lijadiliwe mbele ya mawaziri ili waamue namna ya kupunguza gharama za usafiri wa anga . “Wabunge tunapaswa tufanye Kila Nchi ili wananchi wetu wanufaike na jumuiya yao ya Afrika Mashariki Kwa gharama nafuu za usafiri ndio maana tulijipanga kuwaomba mawaziri waone namna ya kupunguza gharama za anga Kwa Nchi za EAC”amesema. Spika wa muda wa bunge hilo, Abdulkadir Aden amehairishwa bunge hilo Hadi jumanne ijayo ambapo pamoja na mambo mengine Waziri mteule Betty Maina kutoka Kenya anatarajiwa kuapishwa ili awe miongoni mwa mawaziri wa EAC baada ya Waziri aliyekuwepo Aden Mohamed kujihudhulu Kwa ajili ya masuala ya uchaguzi nchini kwao.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: