Kundi kubwa la watalii kutoka Urusi na Poland wakishuka katika ndege kubwa katika uwanja wa Mtemere uliopo ndani ya hifadhi ya Nyerere ikitokea Zanzibar Kwa ajili ya kuja kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi ya Nyerere
Kundi kubwa la watalii wakiwa katika magari maalum ya utalii mara baada ya kushuka uwanja wa Mtemere kwaajili ya shughuli za utalii katika hifadhi ya Nyerere
Afisa mhifadhi anayeshughulikia utalii katika hifadhi ya Nyerere Seth Mihayo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa ni rahisi sana watalii kutoka Zanzibar kuja kutalii Nyerere kwakuwa mwendo ni dakika 40 tu


 Na Pamela Mollel,Nyerere




Ndege kubwa iliyobeba watalii inatua katika uwanja wa Mtemere ulioko ndani ya Hifadhi ya Nyerere, ikitokea Zanzibar.

Wameshuka watalii wapatao hamsini majira ya asubuhi,Baadae ndege nyingine tatu au Zaidi hutua tena ndani ya hifadhi hiyo zikitokea visiwani, kuwaleta wageni wengine kwa ajili ya utalii wa kujionea wanyamapori.

Ndege hizo kwa idadi tofauti, hushuka katika hifadhi hiyo mpya na kubwa zaidi nchini mara mbili au tatu kwa wiki, kutoka visiwani.

Idadi ya ndege na watalii hutegemeana na msimu pamoja na idadi ya wageni husika.

Imebainika kuwa kuna upacha wa ajabu kati ya Hifadhi Mpya ya Nyerere na visiwa vya Zanzibar, kiasi kwamba ndani ya siku moja watalii hutembelea maeneo yote mawili kwa wakati mmoja.

Wageni kutoka Urusi, Poland na nchi zingine za Ulaya ambao hupendelea kufanya utalii wa fukwe, katika visiwa vya Zanzibar, wamegundua kuwa wanaweza pia kutumia siku moja ndani ya hifadhi ya Nyerere, kabla ya kurudi tena Unguja,” anaelezea Seth Mihayo, afisa mhifadhi anayeshughulikia masuala ya Utalii katika hifadhi mpya ya Nyerere.

Kwa mujibu wa mhifadhi Mihayo, ni rahisi sana kwa watalii walioko Zanzibar kufika Nyerere kuliko wao kwenda hifadhi nyingine yeyote nchini, kwani ni mwendo wa dakika 40 tu.

“Na hapa Nyerere, kutokana na uwingi wa wanyamapori, watalii huweza kuona aina zote za wanyama ndani ya muda mfupi sana, na katika sehemu ndogo tu, ingawa eneo la hifadhi yenyewe ni kubwa sana,” aliongeza Seth.

Hifadhi ya Nyerere in viwanja sita vya ndege maalum kwa ajili ya kushusha watalii.

Ingawa ilianzishwa miaka mitatu tu iliyopita, baada ya kumegwa kutoka pori kuu la akiba la Selous, Hifadhi ya Nyerere bado imeweza kuvutia watalii wa kigeni Zaidi ya Laki moja kwa mwaka.


Wakala wa Utalii aliyeko Zanzibar, ambaye ni Raia wa Poland, Tomasz Dworczyk anaeleza kuwa kuna muamko mkubwa wa wakazi wa nchini Polanda kutaka kuja kutalii Tanzania.

“Awali walianza na visiwa vya Unguja na Pemba kwa ajili ya utalii wa bahari na fukwe lakini sasa wamegundua kuwa wanaweza pia kufanya utalii wa wanyamapori bara, hususan katika hifadhi ya Nyerere ndani ya siku moja au masaa machache kisha kurejea tena Zanzibar!” alisema Dworczyk.

 

Share To:

Post A Comment: